MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Wednesday, August 19, 2015

Hii Ndio Nguvu Uliyonayo Ndani Yako Itakayokusaidia Kutatua Jambo Lolote Linalokutatiza

Posted by Makirita Amani  |  at  Wednesday, August 19, 2015 No comments

Habari ndugu msomaji wa Amka Mtanzania , Maisha ni mtihani na kila siku maswali ya mtihani huu huwa tofauti na ya jana au wakati uliopita. Maswali haya yanaweza kuwa magumu au rahisi ukilinganisha na maswali ya mtihani uliopita. Lakini kuwa kwake magumu au rahisi hakumaanishi kuwa mtihani huu haufai kutafutiwa majibu. Uwe mgumu au rahisi majibu ni lazima utafute na kupatia au kukosea kwa jibu ndio huleta matokeo ya kufanikiwa au kushindwa.
 
Kama binadamu tunapitia nyakati ngumu mbali mbali na nyakati hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu. Kuna wakati unaweza kudhani kuwa unapitia wakati mgumu sana, umepatwa na matatizo ambayo yamekuwa ni mzigo mzito na safari ya maisha ukaona kuwa imekuwa mbaya kwakua huwezi kuendelea ukiwa na mzigo huo, lakini baadae ukisikia mzigo au tatizo alilonalo mtu mwingine unaona la kwako ni afadhali.
SOMA; Usiruhusu Visingizio Vikushinde, Visingizio Vipo Kila Siku, Ila Muda Haukusubiri.
Ni kweli kuwa ukubwa wa matatizo unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, lakini kushinda au kushindwa kutatua tatizo ni kazi ya mtu husika. Kuna baadhi ya watu hata tatizo liwe dogo kiasi gani, kwake linakua ni kubwa mno na kuna baadhi ya watu ambao kwao hakuna tatizo kubwa yote ni sawa. Na undani wa watu wanaochukulia matatizo yote kuwa sawa, si kwamba ndani yao wanaona tatizo au changamoto wanayopitia ni ndogo, lakini namna wanavyoitatua ndiyo hufanya tuone kuwa changamoto au tatizo hilo lilikua dogo.
Kuna usemi wa Kiswahili kuwa ”Dawa Ya Jino Kung’oa” Ndivyo ilivyo pia katika matatizo au changamoto. Dawa yake ni kuzitatua. Hata kama changamoto utaiona kubwa kiasi gani fahamu kuwa kinachotakiwa kufanyika ni kuitatua kwani kuiacha hakutaleta afadhali, zaidi ya kuleta madhara.
Kuna nguvu tuliyopewa na Mungu ambayo ipo ndani ya kila mmoja na ukipatwa na tatizo kama utakumbuka kuwa una nguvu hii basi hakuna jambo gumu kwako ambalo litakosa utatuzi. Kama binadamu unapopatwa na jambo ni lazima unashituka, hali yako ya kawaida inabadilika kutokana na mawazo yaliyokuja kichwani baada ya kupata tatizo fulani. Kila unachokiona mbele yako kinaleta sura mbaya. Badala ya kuona watu na vitu vinavyokuzunguka bado ni vizuri kama ambavyo ulikua ukiviona awali, vyote vinakua vibaya. Unaanza kuhisi dunia imekuacha peke yako, unasahau nguvu ya mawazo/fikra iliyopo ndani yako kuwa unaweza kuibadili na kwa kuibadili utaanza kuona vitu na watu wote kama awali na hapo unaweza kufikiri vizuri ni njia gani utaitumia kutatua hali inayokukabili.
SOMA; Njia Tatu Za Kuongeza Ufanisi Wako Eneo La Kazi Na Kuepuka Kupoteza Muda Kwa Hadithi Zisizo Na Msaada Kwako.
Watu wenye uwezo wa kutatua changamoto daima hukumbuka uwezo/nguvu waliyonayo ndani yao ambayo inaweza kubadili hali yoyote ile waliyonayo na kufanya wajisikie vizuri. Kama hukua ukiitumia nguvu hii ili kubadili fikra ulizonazo na kutafuta suluhisho la hayo unayoyapitia fanya hivyo sasa. Fikra au mawazo mazuri ni rasilimali kubwa na muhimu sana katika kutatua jambo lolote lile ambalo linakukabili, liwe dogo au kubwa. Hata kama ukipata ushauri kutoka kwa watu wengine nguvu kubwa ya kutafuta suluhisho inatoka kwako. Namna gani unaona jambo linalokukabili na unafikiri nini kuhusiana na jambo au hali uliyonayo kwa wakati huo.
Makala hii imeandikwa na Esther Ngulwa.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top