Ili kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako ni muhimu sana kwako kuwa na elimu sahihi itakayokusaidia kukubadili wewe na jamii kubwa inayokuzunguka. Unapokuwa na elimu hii inakuwa inakupa uwezo  wa  kukabiliana na changamoto nyingi katika maisha na hatimaye kufanikiwa.

Inakuwa inauma sana na kazi bure kama kusoma elimu ambayo hata haikusaidii wewe kufikisha ndoto zako zaidi ya kukufanya kuwa mtumwa kwa kile unachofanya. Hii ni elimu muhimu sana kwako kuipata kwa sababu hujawi kufundishwa  popote pale iwe shuleni au nyumbani.
Kupitia elimu hii itakusaidia kufikia malengo makubwa uliyojiwekea na itakusaidia pia kujitambua zaidi nakutumia fursa nyingi zilizopo nchini kukufanikisha. Kumbuka hii ni elimu ambayo mtu yeyote ana uwezo wa kuipata kama ataamua na hapa sizungumzii elimu ya chuo kikuu. Elimu hiyo ni ipi ambayo ni muhimu sana kwako kuipata na hutakiwi kuikosa?
Hii ndiyo elimu muhimu sana kwako ambayo hutakiwi kuikosa katika maisha yako yote:-

1.  Elimu ya kupanga na kufanikisha malengo.

Ni muhimu kuwa na elimu hii itakayokusaidia kupanga na kufanikisha malengo makubwa uliyojiwekea katika maisha yako. Watu wengi wanajikuta wanashindwa kutimiza ndoto zao kubwa  na malengo yao kuishia kati kwa sababu ya kukosa elimu hii.
Ni lazima ujue katika maisha yako unataka kuwa nani? Unataka kuwa na nini katika haya maisha? Na unataka kutimiza nini hapa duniani katika uhai wako? Ukiweza kujua namna ya kupanga na kufanikisha malengo yako vizuri utakuwa umejenga uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa.
 

2.   Elimu ya Ujasiriamali.

Watu wengi wanapata shida katika maisha yao kwasababu ya kutokujua vizuri elimu hii ya ujasiriamali. Kuajiriwa peke yake haitoshi jifunze kufanya biashara zako wewe mwenyewe badala ya kutegemea kuajiriwa tu.
Tafuta Semina muhimu na kuhudhuria ambazo zinahusiana na mambo ya ujasiriamali na utakuta unajifunza mambo mengi sana ambayo yatakusaidia kutengeneza pesa zako wewe mwenyewe na kuwa tajiri.
 3.     Elimu ya kuwa na mawazo chanya.
Ukitaka kuishi maisha ya mafanikio makubwa jifunze kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa na mawazo chanya inakusaidia wewe kutimiza malengo yako mengi na utajikuta unaachana na fikra zinazokuzuia kufikia viwango bora vya mafanikio. Hii ni elimu muhimu sana kwako ambayo hutakiwi kuikosa katika maisha yako yote.

 4.     Elimu ya madeni

Kuna watu katika maisha yao yote wanateseka na kuteswa sababu ya madeni. Madeni mengi yamewafanya kuwa watumwa kila siku. Wataalamu wa mambo ya madeni wanapendekeza madeni yako yasizidi asilimia 20 ya mapato yako.
 Kama unadaiwa jifunze kulipa madeni mapema hiyo itakusaidia kuwa huru zaidi na utakuwa na pesa zako mwenyewe hata kama ni kidogo. Kuwa na elimu ya madeni ni muhimu sana kwako kuipata elimu hii hata kwa sehemu.
 5.     Elimu ya kutoa.
Watu wengi wenye mafanikio ni watoaji wakubwa pia. Unapotoa ina maana unajali, lakini unapotoa ina maana pia unaacha nafasi ya kujazwa na kingine kwa zaidi. Jifunze kutoa angalau kwa sehemu katika maisha yako itakusaidia sana kuishi maisha ya mafanikio.
Hii ndiyo elimu muhimu ambayo hutakiwi kuikosa katika maisha yako yote. Kama unashindwa namna na jinsi ya kuipata kwa urahisi elimu hii tembelea zaidi mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na pia unaweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA,hapa utajifunza mambo mengi na kupata elimu itakayokupa ukombozi wa maisha.
Nakutakia ushindi katika safari yako ya mafanikio.
TUPO PAMOJA!
IMANI NGWANGWALU. 0767 048 035/ingwangwalu@gmail.com