MUHIMU KUSOMA;

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwekeza Ili Kuweza Kutengeneza Kipato Kwenye Intaneti.

Habari rafiki? Sheria ya asili inasema kila mtu anavuna kile alichopanda, na hiyo ipo wazi kwenye kila jambo tunalofan...

Monday, August 11, 2014

Hizi Ndizo Fikra Zinazokuzuia Kufikia Viwango Bora Vya Mafanikio!

Posted by Makirita Amani  |  at  Monday, August 11, 2014 No comments

MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI NGWANGWALU WA TANGA TANZANIA.

Ili uwe na mafanikio na kupata kile unachokihitaji ni lazima uwe na mawazo yanayoendana na kile unachokihitaji katika maisha yako. Mawazo uliyonayo ni kila kitu, kwani kila unachokihitaji kabla ya kukipata kinaanzia kwenye mawazo.
Huwezi kupata kitu chochote kile katika maisha yako mpaka kwanza uwe umewaza juu ya kitu hicho na kukizingatia kwa muda fulani. Kadri unavyowaza juu ya jambo fulani unalotaka kulitimiza katika maisha yako ndivyo uwezekano wa kulipata jambo hilo au kitu hicho unakuwa nao.
Mawazo ni muhimu sana katika kufanikisha ndoto. Na mawazo ninayozungumzia hapa ni mawazo chanya ambayo yataleta mabadiliko chanya katika maisha yako. Kama wewe unawaza hasi na unaendelea kuwaza hasi nafasi ya kufanikiwa inakuwa ndogo sana kwako.
Unapozidi kuwa na fikra hizi hasi siku hadi siku utajikuta wewe uko nyuma katika maisha yako siku zote. Haya ni mawazo hatari sana katika maisha yako ambayo unatakiwa kuyaepuka vinginevyo ukiendelea kuyang’ang’ania utakwama. Ni mawazo ambayo yamekuwa yakizuia juhudi zako nyingi unazo zifanya kila siku.
Katika makala hii nitazungumzia fikra au mawazo yanayokufanya ushindwe kufikia viwango bora vya mafanikio. Mawazo au fikra hizo ukiwa nazo katika maisha yako zitakutesa na kweli utashindwa kufanikiwa. Haya ni mawazo ambayo umekuwa nayo siku hadi siku pengine miaka na umekuwa ukiyabeba pasipo kujua.
Hizi hapa ndizo fikra au mawazo yanayokufanya ushindwe kufikia viwango bora vya mafanikio:-
1.Maisha yatakuwa mazuri tu.
Haya ni mawazo potofu ambayo yanakudanganya. Huwezi ukafanikiwa katika maisha yako kama utakuwa umekaa tu.Watu wengi wenye fikra hizi wanategemea maisha ya mafanikio, maisha mazuri, yatakuja kesho, mwezi ujao au mwaka unaokuja, haya ni mawazo ambayo wamekuwa wakiwaza kila mara na wameendelea kuwaza hivyo kusubiri hiyo siku ya mafanikio kwao ambayo haifiki.
Mafanikio yatakuja tu kwa kuchukua hatua muhimu juu ya maisha na sio kukaa tu na kupoteza muda bila sababu ya msingi.Una uwezo mkubwa wa kubadili maisha yako vyovyote vile unavyotaka yawe endapo utaachana na fikra au mawazo haya unayojidanganya mwenyewe kila mara.
clip_image002
2.Hali niliyonayo inanitosha.
Binadamu ndio viumbe pekee Duniani ambao tumepewa nafasi ya kubadili maisha yetu jinsi tunavyoweza. Kwa hali yoyote uliyonayo una uwezo wa kufanya mabadiliko makubwa sana katika maisha yako. Pamoja na uwezo mkubwa tulionao wapo watu wanaoridhika sana na mafanikio waliyo nayo ingawa yanaweza yakawa ni kidogo tu.
Kama unataka kufanikiwa zaidi achana na mawazo haya ya kutosheka na hali uliyo nayo sasa. Uwezo wa kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo na ukawa msaada mkubwa kwa jamii unao. Uamuzi ni wako wa kufanya mabadiliko na kufanya kitu kipya katika maisha yako.
3.Ninahitaji kupata uhakika zaidi.
Wapo watu ambao hawawezi kufanya kitu mpaka waulize kwa watu wengine kama kitu wanachotaka kufanya ni sahihi ama sio sahihi. Kama ndani mwako una fikra hizi zitakurudisha nyuma sana. Kwani wengi unao waulizia watakukatisha tamaa kutokana na maneno watakayokwambia juu ya ndoto uliyo nayo.
Kama una nia ya kweli ya kutaka kubadili maisha yako, fata ndoto zako acha kuulizia ulizia sana juu ya ndoto zako. Watu wengi wenye mafanikio makubwa Duniani hawakuuliza uliza sana juu ya ndoto zao bali walichukua hatua ya kujiamini na kufanyia kazi ndoto zao na kusonga mbele.
4.Tatizo nililo nalo ni kubwa sana.
Wapo watu wanaofikiri wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya udhaifu fulani walio nao na hii sio kweli. Hakuna kitu kinachoweza kukuzuia kufikia ndoto zako zaidi yako wewe mwenyewe. Unao uwezo wa kuwa chanzo au kizuizi cha mafanikio yako.
Tambua unao uwezo wa kufanya chochote kile na hakuna tatizo kubwa ambalo lina uwezo wa kukuzuia kufanikiwa zaidi yako. Wewe ndiye kila kitu unaweza kufanya mambo makubwa hata kama huna elimu ya kutosha kama unavyofikiri kitu cha msingi jenga imani ya kuamini kuwa unaweza.
5.Ni kazi ngumu sana kufanikiwa.
Kila unachokitaka kina gharama yake. Hakuna mkato katika hili ni lazima ulipie gharama ndio ufanikishe ndoto zako. Fanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa, uking’ang’ania mawazo haya ya kuona mafanikio ni magumu kuyafikia, itakuchukua muda mrefu kutimiza ndoto na malengo uliyojiwekea. Badili jinsi unavyowaza juu ya mafanikio na maisha yako ya nje utaona yatabadilika vivyo hivyo.
6.Nimepata hasara nyingi sana.
Hizi ni fikra ambazo umekuwa nazo muda sasa. Unashindwa kufanya mambo mapya na kuweka malengo yako upya kwa sababu ya kuogopa hasara uliza pata huko nyuma. Ninachotaka kukwambia ni kwamba kila mtu anapata hasara kwa sehemu yake. Panga malengo yako na achana na woga usio na maana kisha chukua hatua ya kusonga mbele kutekeleza ndoto zako.
Hayo ndiyo mawazo yanayokuzuia wewe kufikia mafanikio unayoyataka. Fanya mabadiliko katika maisha yako, acha kufata tabia za kujinga zinazokuzuia wewe kufanikiwa kwenye maisha yako. Ansante sana kwa kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na endelea kuwashirikisha wengine kwa ajili ya kujifunza mambo mengi mazuri ya mafanikio.
TUPO PAMOJA!
UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII IMANI NGWANGWALU KWA 0767048035.
KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com
MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top