MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Tuesday, May 10, 2016

Tabia Mbovu Zinazowarudisha Wengi Nyuma Kimafanikio.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Tuesday, May 10, 2016 No comments

Mara nyingi tumekuwa tukisema tabia zako ulizonazo ndizo zinazopelekea maisha yako yawe bora au mabovu. Ni jambo ambalo tumekuwa tukikumbushana kwamba siku zote maisha ya binadamu yanaongozwa na tabia alizonazo binadamu huyo. Kwa mantiki hiyo, ikiwa na maana kwamba kwa kujijengea tabia za aina fulani kwenye maisha yako, ndivyo maisha yako yataendelea kuwa hivyo  kama tabia zako jinsi zilivyo.
Tatizo walilonalo wengi ambalo linakuwa linawasumbua sana ni kule kurudishwa nyuma na tabia zao. Utakuta mtu anauwezo mzuri kabisa wa kutengeneza pesa za kutosha lakini kila wakati anakuwa hana au anaishi maisha ya kimaskini kwa sababu ya kujijengea tabia mbaya. Ili kufanikiwa unatakiwa kutambua mapema tabia zinazo kurudisha nyuma kimafanikio. Je, unajua ni tabia gani zinazokurudisha sana nyuma kwenye maisha yako?
1. Kuamini maisha ni magumu.
Siku zote ukweli wa maisha uko hivi; ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe chanya kwanza. Lakini kwa bahati mbaya wengi wetu hawako hivi. Ni watu wa kuamini sana maisha hasi ikiwa pamoja na kuamini maisha ni magumu. Mara nyingi wengi wetu tumelishwa imani ya kwamba maisha ni magumu sana na kusahau tu kwamba maisha yanachangamoto ambazo zinatakiwa kutatuliwa kila siku.
Ukitaka kuelewa vizuri juu ya hiki ninachosema, jaribu kumuuliza kila unayekutana naye ' Maisha vipi?' Au mwambie 'maisha yanaendaje?'. Wengi kati yao watakwambia maisha ni magumu sana. Kwa kuwa na Imani hii maisha ni magumu inawarudisha wengi nyuma kimafanikio kwa sababu akili zao zote zinaamini ugumu katika maisha basi na ndivyo inavyokuwa.

Acha kuamini sana maisha yako ni magumu.
2. Kuahirisha mambo mara kwa mara.
Pia wengi wanakwama kufikia mafanikia kwa sababu ya tabia ya kuahirisha mambo. Utakuta mtu anauwezo kabisa wa kufanya jambo fulani muda huu lakini unashangaa anaahirisha. Kwa tabia hiyo ya kuahirisha jambo hili leo na lingine kesho, hupelekea mambo mengi kutokufanyiwa kazi. Matokeo yake mwisho wa siku hujikuta kukwama na kushindwa kufanikiwa. Kwa hiyo kuahirisha mambo ni moja ya tabia inayowarudisha wengi kimafanikio bila hata pengine wao kujua.
3. Kulaumu wengine.
Wapo wengine pia ambao maisha yao hurudi nyuma kutokana na kulaumu wengine. Unaweza ukashangaa hili linatokeaje? Sikiliza, unapolaumu wengine unakuwa unaona wao ndio wanajukumu la kubadilisha maisha yako na kusahau kwamba jukumu hio unalo wewe. Wewe ndio unayewajibika kwa sehemu kubwa juu ya maisha yako na sio mtu mwngine. Kama utaendelea kulaumu wengine ndio chanzo cha maisha yako kuwa mabaya, tambua kabisa utakuwa umejibebesha tabia ambayo inakurudisha nyuma.
4. Kujilinganisha na wengine.
Ili uweze kufanikiwa na kufika mbali, acha kujilinganisha sana na watu wengine. Fanya kwa sehemu yako lakini kwa ubora wa hali juu. Ikiwa utaamua kujilinganisha sio mbaya lakini isiwe kupitiliza. Kama utaendelea kujilinganisha sana itakupelekea uendelee kuiga maisha ya wengine sana, ambayo kiuhalisia sio yako. Hivyo, ikiwa unataka kufanikiwa acha kuendeleza tabia hii ya kujilinganisha sana na wengine, itakukwamisha na utashndw kufanikiwa.
Kwa sehemu hizo ni baadhi ya tabia mbovu ambazo zinawarudisha wengi nyuma kimafanikio iwe kwa kujua au kutokujua.
Tunakutakia kila la kheri na ansante kwa kutembelea AMKA MTANZANIA kwa ajili ya kujifunza.
Kwa makala nyingine za mafanikio pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com  

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top