MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Monday, August 24, 2015

AMKA Kila Siku Ukiwa Na Hamasa Kubwa Ya Kufikia Mafanikio Makubwa. Zoezi Moja Muhimu Kufanya Kila Siku.

Posted by Makirita Amani  |  at  Monday, August 24, 2015 No comments

Habari za leo rafiki?
Naamini uko vizuri sana na maisha yako yanaendelea kubadilika na kuwa bora zaidi. Hongera sana rafiki yangu, hiki ndio kitu kikubwa ninachopenda kukiona kwako kwa sababu imani yangu kubwa ni kwamba naweza kupata chochote ninachohitaji kwenye maisha yangu kama nitawasaidia watu wengi kupata kile ambacho wanakitaka. Imani hii nilijifunza kutoka kwa mwalimu wangu mzuri kupitia vitabu Zig Zigler.
Na kama bado maisha yako hayajawa bora tatizo ni nini? Unaweza kuniambia kwa kuniandikia email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz halafu tukasaidiana kama marafiki. Mafanikio yako ndio mafanikio yangu, furaha yako ndio furaha yangu. Karibu sana tufanye kazi hiyo kwa pamoja.
Leo hii nataka nikupe zawadi kubwa sana ambayo itabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa sana. Hii ni zawadi kubwa ambayo nimekuwa naifikiria kwa muda mrefu na sasa nimepata jibu lake, na utaipenda sana, yaani sana.
Tuangalie kwanza changamoto tunayokutana nayo kabla hujaijua zawadi hii kubwa na nzuri ambayo itabadili maisha yako.
AMKA ASUBUHI UKIWA NA HAMASA KUBWA YA KUFIKIA MAFANIKIO KILA SIKU
 
Kuna usemi wa kiswahili unaosema kwamba siku njema huonekana asubuhi. Na mwingine unasema kwamba biashara ni asubuhi, jioni mahesabu. Semi hizi mbili, na nyingine nyingi zinasisitiza sana umuhimu wa asubuhi. Yaani asubuhi ni muhimu sana kwa siku yako.
Hii ni kwa sababu asubuhi ndio muda ambao unaianza siku yako. Kama utaianza asubuhi yako vyema ina maana kwamba utakuwa na siku njema. Na kama utaianza asubuhi yako vibaya basi umeharibu siku yako nzima. Hii ni kweli kabisa kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Asubuhi ni mtaji wako mzuri sana ili uweze kuwa na siku nzuri, yenye uzalishaji mkubwa na furaha pia.
Na unajua mafanikio ya maisha yako yanatokana na nini? Yanatokana na mkusanyiko wa siku zenye mafanikio. Na siku yenye mafanikio inaanza asubuhi. Hivyo basi, tunakubaliana kwamba mafanikio yanatokana na asubuhi zenye mafanikio. Asubuhi ni muhimu sana rafiki yangu, muhimu mno. Ndio maana mimi huwa nalinda sana asubuhi zangu. Ukiharibu asubuhi yangu umeharibu siku yangu nzima.
Sasa kama asubuhi ni muhimu sana kwenye maisha yako, unafanya nini kuhakikisha unafaidi kila asubuhi?
Japokuwa asubuhi ni muhimu sana, lakini wengi tumekuwa tunakubali asubuhi zetu ziharibike. Na asubuhi zetu zimekuwa zinaharibikaje?
1. Kuanza asubuhi bila ya kuwa na mpango wowote. Sasa kama asubuhi tu huna mpango, utakwenda kufanya nini siku nzima? Unapoteza siku yako, wewe unaona ni siku moja tu, kumbe inakuondoa kabisa kwenye njia ya kupata mafanikio.
2. Unachelewa kuamka. Kama jua linachomoza kabla wewe hujachomoza, unategemea nini kwenye maisha yako? Ni kwamba umeamua kuipoteza siku. Kwa sababu unapochelewa kuamka, kila kitu kwenye siku yako kinachelewa na mwisho mafanikio yako yanachelewa.
3. Unaianza siku kwa habari hasi. Unaweza kuianza siku yako mapema, lakini sasa unaianza kwa habari hasi. Unaianza kwa kusikiliza habari za vyombo vya habari au kusikiliza uchambuzi wa magazeti au kusoma magazeti au kuingia kwenye mitandao ambapo kuna habari nyingi za kutisha. Sio habari mbaya kupata ila ni vibaya sana kuzipata asubuhi na mapema. Unaharibu siku yako kabisa, kwa sababu unaanza siku ukiwa na hofu, ukiwa na hali ya kukata tamaa na kushindwa kufanyia kazi mipango yako.
Mambo haya matatu ndio yanayoharibu asubuhi yako rafiki yangu na ndio yanayokuzia wewe kufikia mafanikio makubwa. Najua kwa sababu hata mimi nilikuwa mtumwa wa mambo hayo lakini sasa nimepata ukombozi baada ya kuanza kufanya zoezi dogo sana ambalo ninakwenda kukushirikisha leo.
Je upo tayari kuibadili asubuhi yako ili uwe na siku njema na yenye mafanikio? Kama jibu ni ndio karibu kwenye sehemu ya pili muhimu. Kama jibu ni hapana unaweza kuishia hapa na siku utakapokuwa tayari utakaribia.
Jambo muhimu la kufanya ili kuwa na asubuhi njema na siku yenye mafanikio.
Kama umefika hapa maana yake upo tayari kubadilika, karibu sana na ninakuhakikishia kwamba kweli utabadilika, kama utafanya zoezi dogo ambalo nitakushirikisha. Na kama umesoma mpaka hapa, usiache kufanya zoezi hili.
Kwa sababu asubuhi yako ni muhimu sana, basi ni muhimu uilinde. Na kuilinda asubuhi yako zoezi tunalokwenda kufanya litakuwa na vipengele viwili, kwanza kuamka mapema na pili kuianza siku yako ukiwa na mtizamo chanya, bila ya hofu au kukata tamaa.
Nakwenda kukushirikisha zoezi ambalo litakuwezesha wewe kuanza siku yako mapema na ukishaianza iwe chanya na yenye mafanikio makubwa.
Zoezi hili linakuwa hivi, mimi nakutumia wewe ujumbe mzuri sana wa kuianza siku yako kila siku saa kumi na moja kamili asubuhi. Ujumbe huu unaingia moja kwa moja kwenye simu yako mahali popote ulipo Tanzania na hata duniani. Huu ni ujumbe wa kawaida wa simu na ukishakuwa na namba ya simu tu ujumbe huu unaingia moja kwa moja. Haitaki uwe na mtandao wa intaneti au la, kama unaweza kupokea meseji kutoka kwa watu wengine basi pia utapokea ujumbe kutoka kwangu/amka mtanzania.
Ujumbe huu utakuwa wa kukupa hamasa, wa kukupa changamoto ya kuitumia siku yako vizuri, wa kukufanya ufanye kitu kipya kwenye maisha yako. Na kwa sababu ujumbe huu utakuwa unaupokea kila siku, basi ile hali ya kutegemea ujumbe utaingia itakufanya wewe uweze kuamka mapema ili uweze kuanza siku yako kwa ujumbe mzuri sana.
Yaani nina hamasa kubwa sana rafiki ya kuanza kukutumia ujumbe huu kwa sababu naona kabisa jinsi ambavyo unakwenda kubadili maisha yako, kama ambavyo maisha yangu yamekuwa yanabadilika.
Je unataka kupokea ujumbe huu kila siku? Kama jibu ni ndio basi karibu sana. Nitaweka fomu hapo chini na weka namba yako ya simu unayotumia na utaanza kupokea ujumbe huo mzuri kila siku asubuhi.
Kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha wewe unapata ujumbe huu na hivyo tunatumia mfumo wa kuweza kutuma ujumbe kwa watu wengi, kwa sababu marafiki na wasomaji wangu mpo wengi sana. Na mfumo huu tunaotumia una gharama za kuuendesha. Hivyo basi kama unataka kupata huduma hii utachangia kiasi cha shilingi za kitanzania 170 tu kila siku. Ndio tsh 170/= sijui hata inalingana na nini hiyo gharama, soda? Hapana, biskuti, sijui. Lakini ni gharama ndogo sana ukilinganisha na thamani unayokwenda kuipata.
Hivyo ili kupata ujumbe huu mzuri kila siku utalipa gharama za mwezi mzima ambazo ni tsh elfu tano(5,000/=). Kwa kulipa gharama hii kila mwezi utajihakikishia nafasi ya kuhamasika kila siku na kuianza siku yako ukiwa na hamasa ya kufikia mafanikio makubwa.
Anza kupokea ujumbe huu bila ya kulipa chochote.
Bado una wasiwasi au hujui ujumbe huu utakuwaje? Ondoa shaka, huhitaji kulipa kiwango chochote kwa sasa. Unachohitaji ni kutoa majina yako na namba yako ya simu na utapokea ujumbe huu siku tatu bila ya kulipia chochote, halafu kama utaona ni vyema utalipia, kama utaona sio vyema kwako hutalipia na hutapokea tena ujumbe, na tutaendelea kuwa marafiki, nitaendelea kukuandalia makala nzuri sana zitakazokusaidia kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako.
Utaratibu wa kulipia utakuwa ni kabla ya tarehe moja ya kila mwezi na utapokea ujumbe kila siku kwa mwezi mmoja.
Bonyeza maandishi haya na weka taarifa zako na utapokea ujumbe bure kwa siku tatu, baada ya hapo utafanya malipo ili uweze kupokea ujumbe huu kila siku kwenye maisha yako.
Hiki sio kitu kipya, nimekuwa nafanya hivi kwa wale wanachama wa kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, kila siku saa kumi na moja wanapata ujumbe wa kuianza siku yao na wengi wamekuwa na hamasa kubwa na wameshajijengea utaratibu wa kuamka asubuhi na mapema. Najua sio wote wanaoweza kuwa na wasap na ndio maana nimetafuta utaratibu huu utakaomfaa kila mtu.
Pia unaweza kumwandikisha mtu ambaye ni muhimu kwako na labda hajaijua AMKA MTANZANIA kwa sababu hana mtandao, ila ana namba ya simu. Mwandikishe, lakini mwambie kwanza kwamba atakuwa anapokea ujumbe mzuri kila siku, na unaweza kumlipia siku za mwanzoni na baadae kama ataona ni vyema kwake ataendelea kulipia. Labda ni ndugu au rafiki yako yupo kijijini, anaweza kunufaika sana na huduma hii nzuri ya ujumbe wa kila siku asubuhi.
Hii ni nafasi ya kipekee kwako kuianza siku yako ukiwa na mtizamo chanya na hamasa kubwa sana ya kwenda kuweka ubora kwenye kile ambacho unafanya. Usiipoteze, weka taarifa zako hapa sasa hivi na utaanza kupokea ujumbe bure kwa siku tatu na baada ya hapo utaamua ulipie au la.
Nakutakia kila la kheri rafiki yangu, ufanyie kazi yale ambayo unajifunza ili siku yangu na maisha yako yaweze kuwa bora sana.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
0717396253
Kama bado hujaweka taarifa zako ili kupokea ujumbe, bonyeza hapa na weka taarifa zako.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top