MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Friday, April 10, 2015

KITABU; MEGA LIVING(Siku 30 Za Kuboresha Maisha Yako).

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, April 10, 2015 No comments

Mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu katika kipengele hiki cha vitabu ambapo kila mwezi tunakushirikisha kitabu kimoja kizuri cha kusoma. Vitabu tunavyokushirikisha vinakuwa na maudhui na maarifa ya kukuwezesha kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako. Haya yote yanatokea pale utakapofanyia kazi kile ambacho unajifunza kwenye vitabu hivi.

Mwezi huu wa nne tunakushirikisha kitabu MEGA LIVING ambacho kimeandikwa na Robin Sharma. Robin ni mmoja wa wahamasishaji wakubwa sana duniani. Ribin ameandika vitabu vingi kuhusu uongozi na maendeleo binafsi ya mtu.

Katika kitabu hiki MEGA LIVING utajifunz ambinu zote muhimu za kukuwezesha kubadili sana maisha yako na kuweza kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako kufikia mafanikio makubwa.

Kitabu hiki kimegawanywa kwenye sehemu tatu.

Sehemu ya kwanza inaelezea falsafa ya mega living. Katika sehemu hii utajifunza mambo yote muhimu unayohitaji kujua na kufanya ili maisha yako yawe bora sana. Hapa utajua kwamba kuna uwezo mkubwa uliopo ndani yako na unawezaje kuutumia. Utajua umuhimu wa kuweza kujiongoza wewe kwanza kabla hujamuongoza mtu mwingine. Na pia utakumbushwa umuhimu wa mtizamo chanya kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.

Pia utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka malengo ambayo utaweza kuyafikia kwenye maisha yako.

Utajifunza jinsi ya kuyatumia maeneo muhimu sana kwenye maisha yako ili kuweza kuw ana maisha bora na yenye mafanikio. Maeneo hayo muhimu ni afya, hapa utajifunza jinsi gani ya kula ili uweze kuwa na nguvu siku nzima. Moja ya vitu vinavyokurudisha nyuma ni jinsi ambavyo unakula, vyakula unavyokula na muda unaokula vyakula hivyo. Jambo jingine muhimu utakalojifunza kwenye afya ni jinsi ya kupumua. Kwa sehemu kubw aunakosea sana unavyopumua na hivyo unajichosha na kushindwa kufanya mambo ambayo ni muhimu kwako.

Maeneo mengine muhimu ni imani na maarifa au akili. Katika hili la akili utajifunza jinsi ya kutuliza akili yako na iweze kufanya jambo moja muhimu kwa wakati. Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi sana hivyo kupata utulivu ni jambo muhimu sana.

Kingine muhimu utakachojifunza kwenye sehemu hii ni jinsi ya kuvutia utajiri na mafanikio kwenye maisha yako.

Sehemu ya pili ya kitabu hiki utajifunza siri 200 za kuweza kuboresha maisha yako. Siri hizi 200 zitakufanya uweze kuyabadili maisha yako na kuwa bora kwenye kila idara.

Sehemu ya tatu ya kitabu hiki ina programu ya siku 30 ya kubadili maisha yako na kuyafanya kuwa bora zaidi. Katika programu hii, kila siku utapewa changamoto moja ya kufanya ambayo itayabadili maisha yako.

Soma kitabu hiki na utajifunza mambo mengi sana muhimu na kama ukiyatumia uliyojifunza, maisha yako hayataendelea kuwa kama yalivyo. Kitabu hiki ni kifupi na hata kama hupendi kusoma, kitabu hiki hakichoshi. Kadiri utakavyoendelea kukisoma ndio utazidi kupata hamasa na kuona makosa ambayo umekuwa unafanya na yanakuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Kupata kitabu hiki MEGA LIVING bonyeza hayo maandishi ya kitabu na utakipakua.

Soma kitabu hiki, soma angalau kurasa kumi kila siku na utaondoka na vitu muhimu vya kuboresha maisha yako.

Kama bado hujasoma kitabu JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA hupo makini na maisha yako. Hiki ni kitabu ambacho kimeelezea mabadiliko yaliyotokea, yanayotokea na yatakayotokea kwa siku zijazo. Ni kitabu ambacho kitakuandaa wewe ili uweze kufaidika na mabadiliko yatakayotokea, kwa sababu mabadiliko yapo na yanapotokea watu wengi huachwa nyuma. Tunaishi kwenye dunia ambayo mabadiliko yanatokea kwa kasi sana. Mambo mengi tunayofurahia leo na kuona ndio fursa yatatoweka muda sio mrefu. Kazi unayofanya leo, biashara unayofanya leo miaka mitano au kumi ijayo itakuwa imebadilika sana, je wewe utakuwa wapi? Hakikisha siku ya leo haiishi kabla hujapata na kusoma kitabu hiki. Kitabu kinapatikana kwa soft copy yaani pdf na unaweza kukisomea kwenye compyuta, tablet au smartphone. Kitabu kinatumwa kwa email na gharama yake ni tsh elfu tano. Kukipata kitabu tuma fedha tsh 5,000/= kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu mara moja.

Nakutakia kila la kheri katika kuboresha maisha yako kwa kitabu MEGA LIVING na pia kujiandaa na mabadiliko yanayokuja kwa kitabu; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

mabadiliko cover EDWEB

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top