MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Tuesday, March 3, 2015

TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Kuweka Kipaumbele Kwenye Maisha Yako.

Posted by Makirita Amani  |  at  Tuesday, March 03, 2015 No comments

Miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, kipaumbele pekee cha mwanadamu kilikuwa kula na kujilinda dhidi ya hatari. Katika nyakati hizo chakula kilikuwa kikipatikana kwa kuwinda au kuchimba mizizi. Hivyo mtu aliamka asubuhi akiwa na kipaumbele kikuu ambacho ni kutafuta chakula. Na usiku aliporudi kulala, kipaumbele kilikuwa kujilinda dhidi ya wanyama wakali na hata hatari nyingine zinazoweza kuhatarisha maisha yake.

Miaka ilivyozidi kwenda mwanadamu aliendelea kufanya ugunduzi ambao ulirahisisha maisha yake zaidi. Badala ya kuwinda tu au kuchimba mizizi sasa aliweza kulima na hata kufanya kazi nyingine. Zikaja zama ambapo mtu aliweza kuajiriwa kama mfanyakazi na kipaumbele chake kilikuwa kutimiza majukumu ya kazi.

Sasa tunaishi kwenye zama ambazo masaa 24 kwa siku na siku 7 kwa wiki unaweza kuwa umeunganishwa na dunia. Wakati unasoma hapa kuna jumbe mbalimbali zinakusubiri kwenye mitandao ya kijamii, kuna jumbe nyingine za kujibu kwenye simu, kuna mtu anataka kukupigia simu muongee, kuna mwingine kakutumia picha au video kwenye simu yako anataka uiangalie. Wakati huo huo kuna kipindi kizuri kwenye tv au radio unataka kufuatilia, kuna tamthilia nzuri unataka uiangalie, kuna matangazo yanayokushawishi ujaribu kitu fulani ambacho wanadai ni kizuri.

Ukiacha haya ya mtandao na teknolojia, bado kuna watu wanaokuzunguka ambao wanakutegemea ufanye jambo wanalotaka wao, una wateja ambao wanategemea huduma nzuri kutoka kwako, una bosi ambaye anaweza kukupigia simu muda wowote na kukupa jukumu jipya, una wafanyakazi ambao wanakutegemea wewe uwape maelekezo ya nini cha kufanya.

Kwa kifupi tunaishi kwenye dunia ambayo, kwa muda ule ule, tuna majukumu mengi sana ambayo hatuwezi kuyatimiza yote hata kama tungejigawa mara ngapi. Huwezi kutimiza majukumu yote hayo kwa sababu hakuna muda wa ziada kwa siku na pia huna nguvu ya kutosha kufanya mambo yote hayo.

Unafanyaje katika hali hii?

Katika mvurugano wote huu ndani ya muda mfupi wa masaa 24 unawezaje kupambana nao? Hii ndio changamoto kubwa sana ambayo inawakabili watu wengi. Na changamoto hii ndio inawatofautisha watu waliofanikiwa sana na wale ambao hawajafanikiwa au wanasukuma tu siku.

Mwezi huu wa tatu hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA tutajadili jinsi ya kujijengea tabia ya kuweka kipaumbele kwenye maisha yako. Hii ni tabia muhimu sana ambayo hutakiwi kuikosa kwenye maisha yako kama kweli upo makini na unataka kufikia mafanikio.

Katika kila siku ya jumanne, kwa jumanne tano za mwezi huu wa tatu tutakuw ana makala moja inayoelezea kw akina kuhusu tabia hii ya kuweka kipaumbele kwenye maisha. Makala hizo zitakuwa kama ifuatavyo;

1. Maana ya kuweka kipaumbele.

2. Umuhimu na faida za kuwa na kipaumbele.

3. Jinsi ya kuweka kipaumbele.

4. Tabia zinazoharibu kipaumbele chako kwenye maisha.

5. Uhusiano kati ya kuweka kipaumbele na mafanikio makubwa.

MAANA YA KUWEKA KIPAUMBELE.

Kuweka kipaumbele maana yake ni kuchagua kitu kimoja cha kufanya katika vitu vingi ambavyo unaweza kufanya katika wakati fulani. Hii ina maana kwamba katika wakati wowote ule unaweza kufanya hata vitu kumi, lakini wewe unaachana na vitu vingine vyote na kuweka akili yako yote, mawazo yako yote na moyo wako wote kwenye kufanya kitu kimoja tu. Kitu hiko kinaweza kuwa na manufaa kwako au kisiwe na manufaa.

Changamoto kubwa ya kuweka kipaumbele ni kwamba…

Kuendelea kusoma na kupata makala nyingine zitakazohusu tabia hii jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi, jaza fomu kwa kuweka taarifa zako kisha lipa ada ya uanachama na uendelee kujifunza. Kupata makala hizi za tabia za mafanikio, pamoja na makala za ujasiriamali na biashara ada ni shilingi elfu kumi tu kwa mwaka mzima. Tuma sada hiyo kwenye namba 0717396253/0755953887 pamoja na email uliyojiunga nayo kisha uanachama wako utadhibitishwa. Pamoja na tabia hii ya kuweka kipaumbele, utajifunza kuhusu tabia nyingine muhimu kama kuamka mapema, kujisomea, kutunza fedha, uaminifu, kujiamini na nyingine nyingi.

Kama kuna tabia moja ambayo inaweza kukufanya wewe uendelee kubaki kwenye mstari utakaokufikisha kwenye mafanikio, basi ni tabia ya kuweka kipaumbele. Twende pamoja kwenye mfululizo huu wa makala ili uweze kujifunza jinsi ya kuweka kipaumbele na kukiheshimu.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa zaidi ya uliyonayo sasa.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo432

Tags:
KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top