MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Friday, February 27, 2015

Hapa Ndio Unapoweza Kuwapata Watu Watano Wanaokuzunguka Watakaokuwezesha Kufikia Mafanikio Makubwa.

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, February 27, 2015 No comments

Maisha yako ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka. Hii ina maana kwamba maisha yako yatafanana sana na watu watano ambao unakuwa nao muda mwingi. Watu hawa wanaweza kuwa ndugu wa karibu, marafiki, wafanyakazi wenza, wafanyabiashara wenza na hata watu wowote ambao huwa mnakaa pamoja mara nyingi.

Hii ina maana kwamba mafanikio utakayopata kwenye maisha yako yanategemea sana mafanikio ya wale wanaokuzunguka. Kama wanaokuzunguka wote wana baiskeli, basi na wewe utaishia kuwa na baiskeli na ukijitahidi sana utaishia kuwa na pikipiki iliyochoka.

Kama watu watano wanaokuzunguka ni watu wasiokuwa na maleng, hata kama na wewe utaamua kuwa na malengo itakuwa vigumu sana kuyafikia.

Kama watu watano wanaokuzunguka ni watu wa kukata tamaa na wewe utakuwa mtu wa kukata tamaa.

Chochote kile ambacho utajitahidi kwenda kinyume na watu hawa hawatakuacha, watahakikisha huondoki na utaendelea kubaki nao. Waambie watu hawa kwamba unataka kufanya biashara kubwa, watakuambia huwezi, utashindwa, unapoteza muda. Waambie kwamba unataka ufanye kazi yako kwa juhudi na maarifa ili kuongeza thamani na baadae kuongeza kipato, watakuambia unajipotezea muda, hakuna atakayejali. Nafikiri wewe mwenyewe ni shahidi mzuri wa jinsi ambavyo watu wako wa karibu wamekuwa wakikupa shuhuda mbalimbali za kukatisha tamaa pale unapojaribu kufanya kitu cha tofauti.

Hali hii inatokana na nini?

Hali hii ya kufanana na watu wanaokuzunguka haijaanza leo, imeanza miaka mingi sana iliyopita, zaidi ya miaka 1000 iliyopita. Katika kipindi hiko cha zamani, binadamu alikuwa na majukumu mawili, kuhakikisha amekula na kujikinga na wanyama hatari wa porini. Kwa kuwa mazingira yalikuwa hatari sana, mtu mmoja asingeweza kufanya mambo yote hayo mwenyewe.

Kwa hiyo wanadamu waliamua kuishi kwa makundi na ilikuwa ni hatari sana kuenda kinyume na kundi linavyokwenda. Kama kundi lilikwenda kuwinda, basi wote waliwinda kwa pamoja, ukiamua kwenda mwenyewe ungeweza kukutana na simba mkali na akakufanya kitoweo. Hata wakati wa usiku haikuwa rahisi kulala eneo la peke yako kwa kuhofia wanyama wakali.

Hapo ndipo kufanya jambo kama kundi kulipoanzia.

Sasa hivi ni muda mrefu umepita na hatari zilizokuwepo zamani hazipo tena. Lakini bado watu tumeendelea kungangania asili yetu ya kufanya jambo kama kundi. Na hata mfumo wa elimu, mfumo wa kazi na hata mifumo mingine ya kimaisha inatulazimisha kufanya kitu kama kundi.

Kuna kipindi nilikuwa naongea na kijana aliyetoka mafunzo ya JKT kutaka kujua mambo gani aliyokutana nayo kwenye mafunzo yale ambayo yalimshangaza. Alinieleza mengi na mojawapo ni kwamba huwa wanapewa mitihani, anayefeli kuliko wengine anapewa adhabu na anayefaulu sana kuliko wengine naye anapewa adhabu. Wanafanya hivyo kwa sababu wale wanaopata maksi ndogo sana au kubwa sana kuliko wengine wanaonekana hawana ushirikiano mzuri na wengine.

Katika hali hii ya kufanya jambo kwa kundi ndio inayokufanya ushindwe kuchomoka kwenye kundi ambalo upo sasa. Kila utakavyojiangalia na ukawaangalia wale wanaokuzunguka hakuna tofauti kubwa sana.

Ufanye nini sasa?

Kama unataka kufanya mambo tofauti na unayofanya sasa, kama unataka kwenda mbele kuliko unavyokwenda sasa na kama unataka kufikia mafanikio makubwa kuliko uliyonayo sasa, unahitaji kuanza kuzungukwa na watu tofauti nawanaokuzunguka sasa.

Unahitaji watu ambao watakutia moyo kwa wazo kubwa ulilonalo kuhusu kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio. Unahitaji watu ambao watakupa moyo hata pale utakaposhindwa katika jambo unalofanya na kukufanya uweze kuanza tena.

Unahitaji watu ambao hawatakukatisha tamaa na watakuwa tayari kukusahihisha pale unapokosea.

Changamoto ni kwamba watu hawa unawapata wapi? Watu wenye mtizamo tofauti, watu wenye mafanikio makubwa hawapo wengi sana kwenye kila eneo. Ni watu wachache sana na kwa bahati mbaya hawana muda wa kuanza kukaa na kila mtu na kumpa mambo hayo mtu anayohitaji kupewa.

Njia rahisi kwako kupata watu wapya wanaokuzunguka.

Kuna njia rahisi sana kwako kupata watu wapya wanaokuzunguka wenye mtizamo chanya, wanaoona mbali zaidi na wanaofikiria makubwa. Watu hawa wanaweza kukupa moyo ujaribu na hata kukupa moyo pale unaposhindwa na kukushawishi uanze.

Je ukiwajua watu hawa utakuwa tayari kujiunga nao?

Je ukijiunga nao upo tayari kuboresha maisha yako?

Je ungependa na wewe kufikia mafanikio kwa kuzungukwa na watu ambao tayari wana mafanikio na wanaendelea kuyasaka mafanikio zaidi?

Kama majibu yako ni ndio, ndio, ndio tayari umeshapata nafasi ya wewe kuzungukwa na watu watakaukusukuma kufikia mafanikio makubwa. Unachohitaji kufanya ni kukamilisha hatua chache muhimu ili uweze kupata manufaa haya.

Unaweza kupata watu wanaokuzunguka na watakaokusukuma kufikia mafanikio kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa uanachama wa GOLD. Unapokuwa GOLD MEMBER kwenye KISIMA, kila siku ya juma unapata makala moja nzuri ya kukufundisha na kukuhamasisha uweze kuchukua hatua zaidi. Makala zinakuwa za biashara/ujasiriamali, tabia za mafaniki, mafanikio ya kiwango cha juu na uchambuzi wa vitabu. Pia kwa kuwa kwenye uanachama huu unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la whatsapp ambapo unapata mengi zaidi kutoka kwa watu wanaoelekea kwenye mafanikio na ambao wameshapata mafanikio. Kila siku utapata ujumbe mzuri wa kuanzia siku yako na hivyo kuianza siku ukiwa na mtizamo tofauti na watu wengine wote wanaokuzunguka.

Kuna faida nyingi sana za kuwa kuwenye kundi hili na cha kushangaza zaidi ni gharama ndogo unayohitaji ili kujiunga. Kwa thamani ya vitu unavyovipata kwenye KISIMA CHA MAARIFA GOLD MEMBER ungehitajika kuchangia angalau shilingi elfu moja kwa siku na hivyo kwa mwaka ingekuwa laki tatu na elfu sitini na tano. Cha kushangaza unachangia shilingi miamoja na arobaini tu kwa siku, ambayo ni sawa na shilinge elfu hamsini kwa mwaka.

Sijui ni kitu gani unachoweza kununua kwa shilingi 140 kwa siku, lakini kuna nafasi hii muhimu ambayo ni sawa na bure kwako. Maana kwa siku utakunywa soda ambayo ni zaidi ya shilingi 500 na haina faida yoyote ile kwenye mwili wako(yaani kunywa soda ni sawa na umeongeza uchafu kwenye mwili wako), utakunywa bia ambayo ni zaidi ya shilingi elfu mbili, utafanya vingine vingi ambavyo vina faida kidogo sana kwako. Lakini kwa jambo ambalo litaboresha maisha yako utaona ni ghali kwako.

Jiunge leo na KISIMA CHA MAARIFA, maana kadiri unavyochelewa unazidi kujinyima nafasi nzuri ya wewe kuboresha maisha yako.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye ukombozi wa maisha yako Kujiunga bonyeza haya maandishi KISIMA CHA MAARIFA, jaza fomu na kisha tuma ada ya uanachama tsh elfu hamsini(50,000/=) kwenye namba 0717396253/0755953887 na utume email uliyojiunga nayona unanachama wako utadhibitishwa.

Kama wewe ni BRONZE MEMBER, unahitaji kuongeza tsh elfu 40 ili kuingia kwenye GOLD MEMBER ila kama utaweza kulipia leo natoa ofa ya kulipa tsh elfu 30. hii ni kwa BRONZE MEMBER tu, yaani wale waliojiunga kwa tsh elfu 10. Kama ni SILVER MEMBER unaongeza tsh elfu 20.

MUHIMU; Kwa wale ambao wamejaza fomu lakini hawajakamilisha malipo, taarifa zao zitafutwa baada ya leo, hii inatokana na watu wengi sana kujaza fomu na kutolipia, hivyo idadi ya wanaosubiri inakuwa kubwa. Hivyo kama unakumbuka ulijaza fomu, lipia kabla taarifa zako hazijafutwa.

Tunakusubiri kwa hamu, kwa sababu tunataka wote tufanikiwe kwa pamoja, tulete mabadiliko makubw akwenye jamii yetu.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo432

 

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top