MUHIMU KUSOMA;

SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu, Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikua...

Wednesday, November 5, 2014

Njia Bora Ya Kusimamia Fedha Zako Katika Biashara.

Posted by Makirita Amani  |  at  Wednesday, November 05, 2014 No comments

Habari za siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ni matumaini yangu unaendelea vizuri katika harakati zako za kutafuta mafanikio na uhuru wako wa kifedha .Katika kona yetu ya Ujasiriamali na biashara ,tutaona njia bora ya kusimamia fedha zako katika biashara. Fahamu kuwa, Fedha ni kitu ambacho sisi sote tunakitaka na kukihitaji. Kuzitumia huwa si tatizo lakini kuzizalisha na kuzitunza wakati wote ni jambo lenye changamoto kubwa hasa kwa wafanyabiashara wadogo ambao ni wageni katika uwanja huu wa Ujasiriamali.

Vilevile tambua Kuwa, kuwa mtu mfanyabiashara kunamaanisha kwamba ni lazima huanze kufikiria tofauti kuhusu fedha zaidi ya ulivyokuwa unafanya huko nyuma. Hata linapokuja suala la kutumia, unapaswa kuanza kufikiria mapema na kufanya uamuzi mzuri unaozingatia taarifa sahihi. Pia ni lazima uzingatie kwa umakini suala zima la Mapato na matumizi katika biashara (soma ; Njia Sita(6) Za Kudhibiti Matumizi Yako Katika Biashara ).

Tambua kuwa Katika biashara, fedha huelekea sehemu mbili. Pale zinapoingia kwenye biashara yako zinaitwa mapato. Wakati zinapotoka zinaitwa matumizi. Ili biashara yako izalishe fedha, mapato yako yanatakiwa kuwa makubwa kuliko matumizi.

Kabla ya kufungua biashara unaweza kukadiria ni kiasi gani biashara yako itazalisha (mapato). Unaweza pia kukadiria ni kiasi gani biashara yako itakugharimu (matumizi). Kukadiria hapa ina maana kiasi cha fedha unachodhani biashara yako itakuzalishia au kukugharimu. Ni vigumu kukisia kwa usahihi ni kiasi gani utauza na utatoza bei gani. Watu wengi hukisia bei ya juu sana, halafu hugundua kwamba biashara zao zinashindwa kuendelea. Mwanzoni ni vizuri kukisia kwamba utakuwa na wateja wachache tu.

Fahamu kuwa, Kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara ni jambo muhimu sana na Ili kuweka kumbukumbu sahihi ni vizuri kujua Fedha inayoingia na Fedha inayotoka katika biashara yako

Namna ya kukadiria mapato ya biashara

Mambo matatu muhimu yatakayokusaidia katika kukadiria mapato ya biashara yako

1.Kwanza unatakiwa kukadiria ni wateja wangapi unafikiri utakuwa nao.

2. Utahitaji pia kuandika ni kiasi gani utatoza kwa huduma ya kila bidhaa.

3.Halafu unatakiwa kuzidisha takwimu hizi ili kujua ni kiasi gani utapata kwa mwezi. Kifaa/huduma Idadi ya vifaa Jumla ya mapato

Tambua kuwa Ili biashara yako ifanikiwe, ni lazima izalishe ziada. Hii ni pale mapato yanapozidi matumizi. Iwapo hali ni kinyume chake, kwamba matumizi yako ni zaidi ya mapato, unapata hasara, jambo linalomaanisha kwamba biashara yako haizalishi fedha za kutosha ili kujiendeleza.

Tukutane wiki ijayo kwa makala nzuri zaidi za kujielimisha na kujihamasisha ,daima tupo pamoja katika safari hii ya mafanikio na uhuru wa kifedha.

TUNAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA BIASHARA YAKO NA TUPO PAMOJA .

Makala hii imeandikwa na Geofrey Mwakatika, Unaweza kutembelea blog yake Geofrey Mwakatika kujifunza zaidi.

kitabu-kava-tangazo4323

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top