MUHIMU KUSOMA;

SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu, Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikua...

Thursday, October 9, 2014

Unasahau Sana Kitu Hiki Katika Maisha Yako, Ndiyo Maana Hufanikiwi Kwa Kiasi Kikubwa.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Thursday, October 09, 2014 1 comment

Wiki iliyopita nilipata nafasi ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi kule mkoani Morogoro. Katika hifadhi hiyo nilijifunza mengi ikiwemo maisha ya wanyama, na utajiri ambao Tanzania kama nchi inao kupitia hifadhi za taifa zilizopo nchi nzima. Kwa kifupi, katika safari ile kupitia wanyama nilijifunza vitu muhimu vinavyohusiana na maisha yetu ya maendeleo ya kila siku. 


Moja ya kati ya wanyama ambao nilipenda jinsi anavyoishi ni mnyama anayefahamika kama Nyumbu. Huyu ni mnyama ambae yupo katika jamii ya Nyati, lakini wakati mwingine anafahamika kama “zero brain”. Amepewa jina hili kutokana na jinsi anavyoishi maisha yake kwa kutokuwa na kumbukumbu kwa kile hasa anachokifanya.

Mnyama huyu nyumbu anaweza akatoka pale alipo na kuelekea sehemu nyingine pengine kutafuta maji, lakini hata kabla hajafika hujikuta amesahau alichofata na kurudi kule alikotoka. Kuna wakati ambapo akiwa anafukuzwa na mnyama mwingine hujikuta akigonga kitu kama mti kokote atakapogeukia hata kama kwa adui anayemfukuza huelekea huko huko bila kujali.

Kupitia mnyama huyu Nyumbu, ambaye huwa hana mwelekeo maalum wa kule anakokwenda nilijifunza kitu ambacho kinahusiana moja kwa moja na maisha yetu ya malengo. Wengi wetu ingawa tunakuwa tuna malengo na mipango yetu mizuri huwa tunajikuta hatufikii malengo yetu,  kwa sababu tunakuwa ni watu wa kuishi kama Nyumbu na kujikuta tunapoteza karibu kila kitu katika maisha yetu.

Nimeanza na mfano huo kwa makusudi kukuonyesha jinsi baadhi yetu tunavyoishi. Jiulize mwenyewe ni mara ngapi umekuwa ukipanga malengo yako, na inapofika wakati umekuwa ukiyasahau kutokana na kutokujua mwelekeo maalumu wa kule unakoelekea. Ili uweze kufanikisha malengo yako ni lazima uwe na nguvu ya mwelekeo kwa kule unakokwenda.

  

Kwa bahati mbaya, wengi wetu huwa hatuna nguvu hii ya mwelekeo wa kule tunapokwenda ndiyo maana kila tunapokumbana kidogo tu na changamoto huwa ni wepesi sana wa kupotea na kujikuta malengo yetu tumeyapoteza na kukaa upya tena na kutaka kupanga malengo kwa ajili ya mwaka unaofuata. 

Maisha haya umekuwa nayo kwa muda sasa, umekuwa ukikosa mwelekeo kwa sababu ya kushindwa kujua unatoka wapi, upo wapi na unakwenda wapi katika maisha yako ya malengo. Hiki ndiyo kitu ambacho umekuwa ukisahau sana katika maisha yako, ndiyo maana hufanikwi kwa kiasi kikubwa. Na jinsi unavyosahau kiti hiki umejikuta ukiwa tu mtu wa kutofanikisha malengo yako uliyojiwekea.

Ni mara ngapi kila mwaka unapoanza umekuwa ukifurahia na kusema mwaka huu nitafanya hiki na hiki na hiki, lakini siku zinavyozidi kusonga mbele unajikuta unasahau malengo mazuri uliyojiwekea, hii yote inakuwa inatokana na kukosa mwelekeo katika maisha yako. Kumbuka mpaka leo hii zimebaki siku themanini na nne kumaliza mwaka huu. Umefanya nini mwaka huu ambacho kitakuwa cha kujivunia kwako. ( Unaweza Ukasoma pia  Zimebaki Siku 100 mwaka 2014 Uishe, Fanya Kitu Hiki Kimoja Unufaike Na Siku Hizi 100)

Kama ni kuzunguka umezunguka vya kutosha katika maisha yako, sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko na kusonga mbele. Utaweza kufanya mabadiliko haya katika maisha yako, endapo tu utamudu kuwa na nguvu ya mwelekeo. Unaweza ukawa unajiuliza utaipata vipi hiyo nguvu ya mwelekeo? Hicho ni kitu ni rahisi kabisa. 

Utaipata nguvu ya mwelekeo na kumudu kufikia malengo yako ikiwa utachukua hatua kwa kile unachojifunza kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, lakini zaidi ukijiunga na KISIMA CHA MAARIFA huko utafundishwa kwa undani. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA utafundishwa juu ya kujenga nidhamu binafsi itakayokusaidia kufikia malengo yako.

Kama unataka mabadiliko makubwa ya maisha yako hujachelewa ni kitendo cha kuamua leo na kuchukua hatua ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kumbuka gharama ya kujiunga ni tsh elfu kumi kwa mwaka hapo utapata makala zote ikiwemo za biashara na ujasiriamali.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA jaza fomu na kisha tuma tsh elfu kumi kwa mpesa ( 0755953887) au tiGO pesa/airtel money(0717396253). Hakikisha hupitwi na fursa hii muhimu ya kuboresha maisha.

Nakutakia ushindi katika safari yako ya mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

IMANI NGWANGWALU-0767 048035/ingwangwalu@gmail


Tags:
KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

1 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top