MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Friday, January 24, 2014

Jinsi Ya Kupata Masaa Mawili ya Ziada Kila Siku; UHAKIKA

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, January 24, 2014 No comments

  Kama wewe ni mfuatiliaji na msomaji mzuri wa mtandao huu AMKA MTANZANIA huenda umeshakuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na muda. Kutokana na mambo mengi unayoshauriwa kufanya ili kubadili maisha yako unaweza kuona hayawezekani kwa sababu muda ni kidogo.

  Hebu fikiria unaambiwa ujisomee kila siku, ufanye mazoezi, ufanye meditation, utenge muda wa kuweka mipango yako kwa siku, upate muda wa kupitia mipango yako, upate muda wa kupumzika na pia upate muda kwa ajili ya wale unaowapenda na wanaokupenda. Kwa mambo hayo tu tayari siku imeisha na bado hujaweka muda wa kufanya kazi na muda wa kulala.

  Kwa muda mfupi tulio nao ni vigumu sana kufanya mambo yote hayo kila siku. Unaweza kujiaminisha hivyo ila ni uongo mkubwa sana ambao umekuwa unajidanganya kila siku.

  Ili uache visingizio visivyo na maana leo ninakupa njia ya kupata masaa mawili ya ziada kila siku ambapo unaweza kufanya mambo hayo ambayo yatabadili maisha yako na kuwa bora zaidi.

  Kwanza hebu tuangalie muda wetu kwa siku. Kila binadamu ana masaa 24 kwenye siku moja. Wapo wengi ambao wameyagawa masaa yao kwa masaa nane ya kulala, nane ya kazi na nane ya kupumzika. Kwa vyovyote ulivyoyagawa wewe haijalishi, ila unaweza kuokoa masaa mawili ili kufanya mambo yako.

               MASAA 2

  Ili kupata masaa mawili ya ziada kila siku fanya mambo yafuatayo;

1. Amka nusu saa kabla ya muda uliozoea kuamka kila siku. Utumie muda huo kufanya jambo lenye manufaa kwenye maisha yako kama kujisomea au kuweka malengo na mipango. Na ili uweze kuamka nusu saa kabla ni vyema ulale mapema na ulale usingizi mzuri.

2. Punguza nusu ya muda unaotumia kusikiliza redio, kuangalia tv na kuangalia filamu. Asilimia 80 ya vipindi unavyofuatilia kwenye tv au redio havina msaada wowote kwenye malengo yako ya maisha. Asilimia kubwa ya taarifa zinazokushtua kila siku sio za kweli au zimeongezwa chumvi mno. Hivyo punguza muda huu unaotumia kwenye vyombo vya habari na uutumie kubadili maisha yako.

             KUANGALIA TV

3. Punguza muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook na twitter. Mitandao hii ina ulevi fulani, unaweza kusema unaingia kuchungulia ujue ni nini kinaendelea ila ukajikuta saa nzima unashusha tu kuangalia zaidi. Na asilimia 90 ya unayofuatilia kwenye mitandao hii hayana msaada kwenye maisha yako. Tenga muda maalumu kwa siku wa kutembelea mitandao hii ili kujua nini kinaendelea.

4. Zima simu yako au iweke kwenye hali ya kimya kabisa(wala isitetemeshe). Hapa najua utanipinga sana na unaweza kudhani nimechanganyikiwa. Tumehamishia fikra zetu kwenye mawasiliano hasa ya simu. Mtu unakaa na simu ikiita kidogo tu unakimbilia kujibu bila ya kujali ni kitu gani cha muhimu unafanya. Inaingia meseji ambayo haina hata maana ila inakuhamisha kutoka kwenye jambo la muhimu unalofanya. Najua una madili mengi yanayokuhitaji kupatikana kwenye simu ila kuiweka simu yako mahali ambapo huwezi kuiona kwa masaa mawili kwa siku haiwezi kukupotezea dili lolote. Muda ambao unafanya kazi inayokuhitaji ufikiri sana na uwe na utulivu hakikisha simu yako haiwezi kukuondoa kwenye kazi hiyo. Hivyo izime au iwe kimya kabisa na iwe mbali.

  Kila mtu ana masaa 24 kwa siku ila kuna wanaofanikiwa sana na kuna ambao wanaishia kulalamika kwamba hawana muda. Kama una jambo ambalo ni muhimu kwako lazima utapata muda wa kulifanya. Tumia njia hizo hapo juu kuokoa muda unaopoteza kila siku na uanze kuwekeza kwenye maisha yako.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top