MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Wednesday, February 24, 2016

Hatua Muhimu Za Kukusaidia Kutatua Tatizo Ulilonalo.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Wednesday, February 24, 2016 No comments

Siku zote katika maisha ya mwanadamu changamoto au matatizo ni kitu ambacho hakikwepeki. Kila mara binadamu huyu huweza kukutana na changamoto au matatizo haya kwa njia mbalimbali. Wapo ambao wanapokutana na changamoto huweza kuzikabili kirahisi na wapo ambao hukwama kabisa.
Najua na pia naamini kabisa kwa namna yoyote ile umeshawahi kukutana na matatizo katika maisha yako tena hata bila ubishi hata kidogo. Hakuna mtu ambaye hajawahi kukutana na tatizo au changamoto. Kitu cha kujiuliza ulipokutana na tatizo hilo ulifanyaje? Ulikata tamaa au ulisonga mbele?Ni kitu gani ambacho ulifanya?
Katika siku ya leo tutaangalia njia rahisi ambazo unaweza ukazitumia kukabiliana na matatizo hasa pale unapokutana nayo. Njia hizi zitakusaidia sana uweze kutambua kuwa unaweza kufanikiwa hata kama una matatizo. Na pia utaelewa kuwa na matatizo siyo mwisho wa mafanikio. Sasa twende pamoja kujifunza.
1. Amini kila tatizo lina njia ya kutokea.
Inawezekana unaona tatizo ulilonalo ni kubwa sana kiasi cha kwamba halina dawa, lakini si kweli kila kitu kina mwisho wake, ikiwa pamoja na tatizo lako hilo. Kama lilivyoanza ndivyo hivyo  litakavyoisha kitu cha kuzingatia kuwa mvumilivu, ingawa maumivu kweli yapo.

TATIZO ULILONALO LINA MWISHO WAKE.
2. Tuliza akili yako.
Wakati unatafuta suluhisho la tatizo lako jitahidi sana kutuliza akili yako. Mara nyingi akili huwa haifanya kazi vizuri sana kama upo kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Hivyo ili uweze kupata majibu sahihi ya kile unachokitaka ni vyema ukaituliza akili yako ili ikupe majibu sahihi.
3. Acha kutafuta majibu ya kulazimisha.
Kwa vyovyote vile tatizo ulilonalo najua lina kukera na hutaki kabisa kuendelea nalo. Sasa hapa unatakiwa kuwa mwangalifu na kitu kimoja, tafuta majibu sahihi. Acha kulazimisha majibu ambayo yanaweza yasiwe msaada kwako. tumia akili yako vizuri kupata majibu ya kweli.
4. Andika kila njia unayoona inaweza kutatua tatizo lako.
Najua unaweza ukawa una majibu kichwani unayoamini yanaweza yakakusaidia. Sasa hayo majibu unayoyaamini yanaweza kutatua tatizo lako yaandike. Yafanye majibu hayo yawe wazi ikiwezekana yaweke sehemu ya wazi, ili yaumbike vizuri kichawani mwako na kukupa majibu halisi.
5.  Jiamini.
Itakuwa ni kazi bure unatafuta namna ya kutatu tatizo lako wakati huo huo hujiamini. Ni vizuri ukajiamini wewe mwenyewe kwanza na ukajua un uwezo wa kulitatua taizo hilo. Bila ya kujiamini itakuawa ngumu kulitatua tataizo lako na litachukua muda mrefu.
6. Tafuta msaada.
Hilo tatizo ulilonalo sio wewe wa kwanza kulipata. Kama ni hivyo basi tafuta msaada kwa watu wengine ambao walishawahi kupitia hali kama yako. Huwezi hiyo soma vitabu vinavyoweza kukusaidia kuhusiana na tatizo lako. Vinginevyo ukibaki peke yako itakuwa ni ngumu sana kuweza kulitatua kiurahisi.
7. Fanya tahajudi (Sala)
Katika kipindi ambacho upo kwenye maatatizo ni vyema ukajijengea utaratibu wa kufanya tahajudi au sala. Hiyo itakusaidia sana kuituliza akili yako na pengine hata kukupa majibu unayotaka moja kwa moja. Sala pia au tahajudi ina nguvu kubwa sana katika akutatua tatizo ulilonalo.
Kwa kufuata hatua hizo, kwa namna moja au nyingine zitakusaidia kuweza kukabiliana na tatizo ulilonalo. Kitu cha muhimu kwako ni kuweza kuchukua hatua na kusonga mbele.
Ansante kwa kuwa pamoja nami, kwa makala nyingine za maisha na mafanikio pia tembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. 
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top