MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Monday, December 28, 2015

Nimerudi Na Mengi Mazuri Kwa 2016 Usikose Haya Mazuri.

Posted by Makirita Amani  |  at  Monday, December 28, 2015 No comments

Habari za wakati huu rafiki?
Naamini uko vizuri sana na katika msimu huu wa sikukuu hujasahau lile lengo lako kubwa kwenye maisha.
Juma lililopita nilikuwa kwenye likizo kwa utaratibu niliojiwekea wa kuwa na wiki moja ya likizo kila mwaka. Na katika wiki hii nakuwa natafakari kazi niliyoifanya kwa mwaka mzima, na kuona ni wapi pa kuweka mkazo zaidi kwa mwaka unaoanza pamoja na yapi ya kuacha kwa mwaka huo.
Mwaka huu nilipata nafasi hii nzuri ya kuwa na likizo hii ya wiki moja, ambayo ilianza tarehe 19/12/2015 mpaka tarehe 26/12/2015. Katika wiki hii ya likizo nimepata kujifunza mambo mengi sana kuhusu mimi binafsi na mambo ninayofanya.
Na haya mengi niliyojifunza yatafanya AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA kuwa bora zaidi na kuweza kutusaidia wote kuwa na maisha bora sana kwetu.
Nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe msomaji wangu kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi katika kipindi chote hiki. Naamini tupo pamoja kwa sababu kuna mambo mazuri ambayo unajifunza na kufanyia kazi na ukaona matunda mazuri.
Nikusihi tuendelee kuwa pamoja na tuendelee kujifunza na kuchukua hatua, ili maisha yetu yaendelee kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa. Kila mmoja wetu anayo haki na nafasi ya kuwa na maisha bora kadiri anavyotaka, ila muhimu anachohitaji ni kuchukua hatua, yeye mwenyewe, kwa sababu hakuna mtu yeyote anayeweza kukuletea maisha bora popote ulipo. Unayafanyia kazi wewe mwenyewe. 
Mwaka 2016 kuna mengi sana mazuri yatakujia kwenye AMKA MTANZANIA na zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Tuendelee kuwa pamoja na nitaendelea kukushirikisha kadiri muda unavyokwenda.
Naweza kukuahidi kitu kimoja kikubwa rafiki yangu, kama tutakuwa pamoja, kama utaendelea kujifunza na kuyafanyia kazi yale uliyojifunza, basi maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa. Ni lazima utaona mabadiliko kwenye maisha yako na yatakuwa bora sana. Inaweza isitokee mara moja, lakini kama utaendelea kuweka juhudi, ni lazima itatokea.
Jambo moja muhimu sana la kufanya.
Naomba pia nichukue nafasi hii kukukumbusha jambo moja muhimu sana la kufanya wiki hii. Mwisho wa wiki hii yaani tarehe 02/01/2016 ndio siku ya mwisho ya kujiunga na semina yetu kubwa na nzuri ya 2016 NI MWAKA WANGU.
Hivyo kama mpaka sasa bado hujajiunga na semina hii nzuri sana kwetu wote ambao tunataka kufanya mabadiliko makubwa kwetu kwa mwaka huu 2016, fanya hivyo sasa.
Ili kujiunga bonyeza maandishi haya na jaza fomu kwa kuweka taarifa zako. Kisha baada ya kujaza fomu fanya malipo ya semina ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=). Malipo yanafanyika kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887 na TIGO PESA au AIRTEL MONEY 0717 396 253 kwenye malipo jina litakaloonekana ni AMANI MAKIRITA.
Kama tayari ulishajaza fomu basi fanya malipo ili uweze kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwako.
Muhimu zaidi kuzingatia.
Hii ni semina muhimu sana ambayo kama upo makini na maisha yako, na unataka kwenda mbele zaidi basi hutakiwi kuikosa.
Nafasi za kushiriki kwenye semina hii ni chache na hivyo unavyojiandikisha na kutuma ada yako mapema ndivyo unavyojihakikishia ushiriki wako.
Mwisho wa kujiunga ni tarehe 02/01/2016, baada ya hapo hutapata tena nafasi hiyo, hivyo jitahidi sana kuchukua hatua sasa. Watu wengi wamekuwa wanakuja baada ya muda wa kujiunga kuisha, hii imekuwa inaleta changamoto kubwa na kupelekea wao kukosa nafasi za kushiriki kwenye semina hizi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu semina hii, ikiwa ni pamoja na mada zitakazofundishwa na kuzifanyia kazi bonyeza maandishi haya; Karibu Kwenye Semina; 2016 NI MWAKA WANGU WA UBORA WA HALI YA JUU.
Usikose nafasi hii muhimu sana kwako rafiki yangu ya kuhakikisha maisha yako yanaendelea kuwa bora zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
0717396253

Tags:
KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top