MUHIMU KUSOMA;

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwekeza Ili Kuweza Kutengeneza Kipato Kwenye Intaneti.

Habari rafiki? Sheria ya asili inasema kila mtu anavuna kile alichopanda, na hiyo ipo wazi kwenye kila jambo tunalofan...

Thursday, September 17, 2015

Wakati Wa kubadilisha Maisha Yako Ni Sasa, Acha Kusubiri Tena.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Thursday, September 17, 2015 No comments

Naamini umzima wa afya na unaendelea kufuatilia matando huu wa AMKA MTANZANIA kwa ajili ya kujifunza na kuboresha maisha yako. Kama iko hivyo ni sawa, nami nakukaribisha kwa moyo mkunjufu ili kuweza kujifunza zaidi kile tulichokuandalia kwa siku ya leo. Kumbuka maarifa hayana mwisho kila siku ni muhimu kwetu kujifunza  ili kukabiliana na mwendo kasi wa maisha.
Katika siku yetu ya leo ningependa nianze kwa kukuuliza swali hili, ni muda upi ambao unataka kubadilisha maisha yako kabisa?Inawezekana kuna wakati unaweza ukawa unajidanganya nakusema nitafanya hiki ama kile kesho au baada ya muda fulani na huku ukiendelea kusubiri na kufikiri huo ndiyo muda sahihi kwako. Ikiwa uko hivyo, ninachotaka kukwambia unajidanganya na unaendelea sana kupoteza muda wako kwa kusubiri huko.
Kama ulikuwa ukifikiri maisha yanakusuburi, naomba leo ubadili mtazamo wako mara moja na kujua kuwa maisha yako yanakutaka usonge mbele zaidi ya hapo ulipo sasa. Ni wakati wa kujitoa mhanga na kufanya mambo yote yaliyo muhimu ya kuweza kutimiza mipango na malengo yako uliyojiwekea katika maisha yako.
SOMA; Je, Hayo Unayoishi Ndiyo Maisha Yako Halisi?
Huu si wakati wakutulia kusubiria mambo fulani yakutokee, ni wakati wa kusukuma kwa nguvu zote mpaka mafanikio unayoyahitaji yatokee. Sasa umefika wakati wa kuachana kung’ang’ania yale mambo yote yanayokukwamisha na kukurudisha nyuma na kuendelea mbele bila kuzuiliwa na kitu chochote kile.
Wakati ulionao sasa ni wakati wa kuibadilisha duniani uliyonayo na kuishi dunia mpya ya mafanikio. Jaribu kufikiri ndoto zako nzuri ulizokuwa ukizifiri kwa muda mrefu. Je unavyoona utazitimiza lini? Acha kuumiza na kusumbua kichwa sana, wakati wa kutimiza ndoto na mipango yako ni sasa ila tu kwa kuamua kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua.
Kwa kuwa bado una ndoto, muda, nguvu na dira nafasi ya kufanikiwa mpaka hapo sasa unayo tena kubwa hata kama unaona mambo yako yameenda vibaya sana. Acha kujiwekea visingizio vingi na kulalamika kusikokwisha hayo yote hayawezi kukusaidia badala yake chukua hatua zinazostahili kuweza kubadilisha maisha yako kwa nguvu zote.
Mpaka hapo tayari upo nyuma kimafanikio. Kama unafikiri natania jaribu kuangalia wenzako wako wapi sasa. Pia je jiulize hayo maisha uliyonao unastahili kuwa nayo ama umeyapata kutokana na kushikilia makosa ambyo yanakukwamisha sana kila siku. Acha kujitetea kwa lolote huo ndiyo ukweli unaotakiwa kuujua hata kama ukikuumia lakini mabadiliko kwako yanahitajika tena ya nguvu.
SOMA; Sababu Tano Kwanini Wewe Ni Muhimu Sana Kutimiza Malengo Uliyojiwekea.
Ishi maisha yako yako sasa ukiwa kama unayetafuta ushindi. Acha kuishi maisha ya hofu ambayo yanakufanya ushindwe kuchukua hatua sahihi za kuweza hata kujitoa mhanga ili kutimiza ndoto zako. Jitoe, jitoe, nasema jitoe ili kuhakikisha ndoto zako zinatumia kwa namna yoyote na kuwa tayri kulipia gharama hizo muhimu.
Muda sasa ulionao ni wa kufanya kazi kwa bidii, kujituma zaidi na kuhakikisha unayapata maisha unayoyata kuwa nayo. Haiwezekani wengine wawe ndiyo wenye mafanikio halafu wewe ukashindwa kuyafikia. Uwezo wa kubadilsha maisha yao unao  ikiwa hilo utalichukulia kwa umakini wa hali juu.
Unaweza ukajiuliza sasa unaanzia wapi hiyo ni rahisi sana. Kuanzia leo jiwekee kiapo cha kuwa sasa mimi nimeamua kubadili maisha yangu kabisa na sitasubiri chochote na nitaanza na vile nilivyonavyo. Ukishafanya hivyo kisha chukua jukumu zima la kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA huko utakutana na familia nzima ya WANAMAFANIKIO ambapo utapata nafasi ya kujifunza mengi kupitia watu waliofanikiwa.
Kupata maelezo ya namna unavyoweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA  bonyeza hayo maandishi, kisha yakishafunguka fuata maelekezo.
Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuboresha maisha.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 048035,
dirayamafanikio@gmail.com

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top