MUHIMU KUSOMA;

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwekeza Ili Kuweza Kutengeneza Kipato Kwenye Intaneti.

Habari rafiki? Sheria ya asili inasema kila mtu anavuna kile alichopanda, na hiyo ipo wazi kwenye kila jambo tunalofan...

Sunday, September 20, 2015

Unaweza Kuamua Kujifunza Hata Unapotofautiana Mtazamo Na Wengine.

Posted by Makirita Amani  |  at  Sunday, September 20, 2015 No comments

Katika wakati huu tulio nao ni kawaida kukuta watu hawaelewani kabisa na pengine wanatoleana maneno machafu kabisa kwa kuwa tu wametofautiana mtazamo juu ya jambo fulani. Au labda pengine kwa kuwa mwingine kapenda hili na huyu kapenda kile basi huko kutofautiana kunaonekana kama tatizo kubwa kwao, wanashindwa kukubali kutofautiana. Watu wanaenda mbali na kusahau kuwa hata baada ya tofauti hiyo wanayokabiliana nao wanatakiwa kutambua kuwa kuna maisha baada ya hapo, maisha lazima yaendelee tu.
JIFUNZE KUPITIA MTAZAMO WA WENGINE
 
Katika maisha haya tunayoishi hakuna namna utakuwa na mtazamo sawa na watu wengine katika kila kitu, kutofautiana kupo na kutakuwepo tu hamna na namna tutazuia hili. Ni wajibu wetu kujua ni namna gani tunakabiliana na changamoto hii. Unaweza kuamua kutumia kutofautiana kama namna ya kujifunza zaidi kuhusu wengine wanavyopokea changamoto au mawazo tofauti na wanavyoamini au walivyoaminishwa. Mwingine anaweza kuwa ana mtazamo fulani na ana sababu na hoja za nguvu kabisa za kumfanya aamini anavyoamini, lakini mwingine yeye yupo tu au anaamini kwa kuwa ameona ndugu zake wanaamini hivyo au anaona kila mtu anaona hivyo, huyu anakuwa hana sababu ya msingi, naweza sema anafuata mkumbo tu, au mwingine anaweza kuonekana ana mtazamo fulani kwa sababu ya hofu tu, ndiyo mwingine anaogopa kuonekana anaona jambo lile lile tofauti na mtu fulani, anaamini kutofuatiana mtazamo juu ya jambo fulani na watu fulani basi ni kosa kwake, au mwingine yeye naweza kusema ni kama hajielewi, yaani mtu huyu hajui yeye ni nani , yupo tu ili mradi yupo na kuna watu anawaangalia , kila wanachoona ni sawa naye yumo tu, au hata akiona tofauti basi anaona ni utovu wa nidhamu kuwahoji anajikuta analazimika kukubaliana nao tu , hata kama ndani mwake anasikia sauti nyingine kabisa, anaamua kuidhulumu nafsi yale kwa hofu ya kutofautiana na watu wake wa karibu.
SOMA; Mambo Nane(8) Yatakayokufanya Uwe Na Fikra Chanya Kila Wakati Ili Uweze Kufikia Mafanikio.
Lakini pale unapokuwa umetofautiana mtazamo na wengine waweza kuamua hata kuwauliza wakusaidie au kukuambia ni kwa nini wanaona wanavyoona. Kwa watu ambao wapo tayari kwa mijadala mnaweza mkajadiliana vyema na mwisho wa siku wote wawili mkafaidi zaidi kwa kuongeza maarifa. Ikitokea mhusika hayupo tayari kujadiliana bado kuna namna nyingi ya kuweza kukufanya uchunguze zaidi na kujifunza zaidi ili kugundua kuwa ni kwa nini anaona anavyoona kuwa ni sahihi, ni kwa nini anaamini hivyo anavyoamini, kama unaweza kusoma zaidi, soma, fanya utafiti wako kwa namna yoyote ile ili mradi uweze kupata majibu sahihi juu ya kile unatafiti, ili uweze kupata faida katika kule kutofautiana kwenu. Katika kufanya hili epuka kutoka nje ya hoja.
Pale tunapotofautiana ni wakati mzuri sana wa kuweza kuona watu katika uhalisia wao. Kuna maeneo ukimgusa mtu ni lazima hata kama alikuwa anaigiza kuwa yu namna fulani atajikuta tu ameshakuwa vile alivyo kiuhalisia, utaweza kumsoma na kumwelewa vizuri kabisa kwa kuona namna anavyokabiliana na changamoto hiyo. Kuna watu wengine wao wanataka tu uwe kama yeye, uone aonavyo, uamini aaminivyo ikitokea ni kinyume tu basi hamuelewani na waweza kuonekana kama adui kwa mtu huyo, maana mtu kama huyu ukimhoji tu yeye hachukulii kuhojiwa vizuri anaona kama unampinga yeye kama yeye na si hoja mezani. Ni vema kumwelewa mtu huyu ili wakati mwingine unajua uongee naye vipi na amani iendelee kuwepo. Lakini pia wapo wengine wao wanapenda changamoto hawa ni wazuri zaidi maana ukijua kumtumia mtu kama huyu unaweza kujifunza mengi zaidi kwake.
SOMA; Kosa Kubwa Ambalo Waajiriwa Wengi Wanafanya Na Linawazuia Kufanikiwa (Kama Umeajiriwa Usiache Kusoma Hapa).
Kuwa mtu wa kutochukulia kitu kibinafsi, mtu akisema kitu chukua hicho kitu kipime na uone kama kinafaa au la usiwe mwepesi kumvamia aliyetoa hoja hiyo na kuacha hoja pembeni hauwezi kujifunza mengi kwa mtazamo huo. Kuwa na moyo wazi, uwe tayari kujifunza katika kila hali, maana mimi naamini katika kila hali au tukio linalotokea huwa lipo jambo jema la kujifunza haijalishi hilo jambo ni zuri au baya, ni chungu au tamu lazima kiwepo cha kujifunza tu. Uamuzi wa kujifunza au kutojifunza ni wako.
Mimi nimechagua kujifunza katika kila hali na huwa nahakikisha sitoki kapa, sijui mwenzangu umechagua nini.
Makala imeandikwa na Beatrice Mwaijengo.
+255 755 350 772

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top