MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Saturday, September 19, 2015

Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapohitajika Kuzungumza Mbele Ya Wengine Na Ukakosa Cha Kusema.

Posted by Makirita Amani  |  at  Saturday, September 19, 2015 No comments

Umeamkaje rafiki na msomaji wa makala za Amka Mtanzania, ninajua kusudi lako la kuingia humu sio kuja kusoma salamu zangu za kukusalimia wewe bali naelewa unatamani kujifunza jambo jipya, kama ni salamu umesalimiwa sana, inaweza kuwa kabla hata ya kufungua hii makala umekutana na salamu zako kama mbili tatu hivi tangu uamke, sasa na mimi ni lazima nikusalimie japo sio muhimu sana ila ni muhimu ninapokutana na mtu aliyenizidi/niliyemzidi umri au mtu ninayeheshimiana naye, ni tabia ambayo nimekua nimeikuta na sijaona ubaya wake kuiendeleza katika maisha yangu.
Basi Nisikuchoshe na maneno mengi, niende moja kwa moja kwenye somo letu, naamini katika maisha yako umewahi kukutana na jambo hili ambalo naenda kuliongelea hapa punde katika makala hii, umewahi kwenda sehemu na wenzako ama ukawa kwenye kusanyiko la watu wengi, mwenzako akawa anazungumza na wenzako, na katika kuzungumza kwake akawa anagusa point zako cha kushangaza zaidi watu wakawa na mwitikio na msisimko mkubwa wa kuendelea kumsikiliza yeye na wewe uliyeambatana naye una nafasi yako ya kuzungumza baada ya kutoka yeye, ukijiangalia hufahamiki sana, huna jina kubwa la kukufanya watu wawe makini na wewe ki ujumla watu hawajakuzoea kwenye macho yao wala kwenye masikio yao ni mgeni. 


SOMA; SEMINA; MIMI NI MSHINDI (Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu)
Unaweza kutamani ardhi ipasuke uingie chini maana unaona huna cha kuongea, unajihisi kama unaenda kujiaibisha tu mbele za watu, kibinadamu unaona watu walio mbele yako si watu wakuongeleshwa maneno tu ilimradi umeongea, ni watu ambao wapo makini sana kwa mwonekano wao, kinachoendelea kukuchanganya zaidi muda huo, hujawahi kusimama kwenye halaiki kubwa kiasi hicho zaidi labda huwa unakutana/kuongea na watu mliozoeana nao labda  wewe ni mwalimu wa shule, umezoea tu kuonana na wanafunzi wako madarasani kwenye vipindi na paredi, sasa leo hii umealikwa sehemu maalum kwenda kuwahutubia walimu/wafanyakazi wenzako ndani/nje ya nchi wakati bado hujasimama kuongea mwenzako anasimama kuongea vitu vya mhimu zaidi ya wewe ulivyopanga kuongea, ile hofu ya mazingira uliyokutana nayo na maandalizi yalivyo, ndani mwako unajisikia ‘kupaniki’ na kuona ulichopanga kuongea hakina umuhimu tena.
Nikutie moyo kwamba hakuna kitu cha kipuuzi ulichokipanga wewe kuwapa watu, hofu uliyonayo ni kwamba hujiamini kama wewe unaweza ukaongea kitu kilekile kwa utofauti kabisa hata kama mngepangwa watu elfu moja kuzungumzia kitu kimoja bado yatazalishwa maneno tofauti kabisa, unatakiwa kujua ulichokiandaa ni cha thamani kubwa mno, unatakiwa kuendelea kutamani watu wakijue na si kuendelea kufikiri utasema nini, unatakiwa kuendelea kujaza point zako kwa kusikiliza maneno ya wengine na si kuendelea kuwaza wewe kiwango chako cha kuchambua mambo ni mdogo, utakuwa unajiharibia mwenyewe.

Usifanye kosa hili mbele za watu, usisimame mbele za watu wakiwa hawajawahi kukusikia popote pale  ukaanza kusema wasikuangalie wewe ulivyo maskini, ulivyo hujavaa vizuri, ulivyo na elimu ndogo, aliyetangulia kuongea humfikii, yaani ulivyo tu unawaambia watu waliotenga muda wao kukusikiliza, kufanya hivyo utawafanya watu waanze kukushusha thamani yako na kuanza kusema si bora yule aliyeondoka angeendelea kuongea tu mbona huyu amekuja na malalamiko ya kutuchosha tu hapa sisi tumeacha kazi zetu!!. Sasa ukija kuanza kuongea na ukawa huna kitu cha kuwafanya watu wawe makini na unachokizungumza, utaona tu kila mmoja yupo bize na shughuli zake mwingine utamwona ameinama tu chini, mwingine utamwona anasinzia, utahangaika kuwachangamsha kwa kuwaambia wafanye kile unachoona kinafaa wewe lakini hakuna mwitikio zaidi wowote, Lakini mwenzako aliyepita ulikuwa unasikia na kuona anaambiwa ‘endeleaaa mkuuuu’.
SOMA; Mambo 8 Ya Kufanya Kama Kile Unachokifanya Hakikupi Matokeo Unayoyataka.
Unafanyaje sasa unapojikuta kwenye hali kama hii?
Cha kufanya ni hiki hapa, siku zote usijidharau ulivyo na usimdharau yule aliyekutangulia kiuwezo, awe ana uwezo mkubwa wa kukusanya watu na wakamsikiliza, awe ana jina kubwa ambapo hata mtoto wa darasa la kwanza anamfahamu, hiyo isikupe shida huyo ni binadamu wa kawaida kama wewe na bado hajawa Mungu, kilicho ndani yako ni kikubwa, na chake pia ni kikubwa ndio maana wote Mungu aliwaruhusu kuwepo hapa duniani, yaani mkubwa wenu ni mmoja tu.
Cha kufanya usianze/usifikiri kumponda mwenzako kwa maneno mabaya ama usianze kujishusha kwa maneno mabaya, unachotakiwa kufanya kwa wakati huo ni kuingia na kumsifia yeye kwanza, eleza jinsi ulivyomkubali kwa maneno yake, eleza kama hawatafuata kile amekisema hawatafikia malengo yao, unaweza pia ukaingiza sifa zake za huko nyuma jinsi alivyofanya mambo makubwa, kufanya hivyo unawafanya watu wawe makini sana na wewe katika kukusikiliza, na wakati wanaendelea kukusikiliza ghafla unaingiza mada yako. Nakwambia hata kama uwe mtu mwenye hofu kiasi gani, itaondoka hata kabla hujaanza kusema kile umekikusudia maana utaona watu wanavyokufurahia kwa maneno yako ya utangulizi. Nakusisitiza tena, aliyekutangulia amekutangulia usitumie nguvu kubwa kumsema vibaya mbele za watu ili wewe kujiosha, huwezi kujua upendo wa watu juu yao huyo mtu ukoje ukiwa hivyo hutoweza kuingia na maneno mazuri ya kumpongeza kwa kazi zake na watu wanaweza wakakuchukia vibaya sana.

Tumia wengine kufikia malengo yako, usitumie wengine kujidharau na kujiona wewe huwezi, ama kujiona wewe ni msindikizaji tu, wewe ni wa mhimu sana, hupaswi kuhangaika kuwadharau wengine ili wewe uonekane unaweza bali tumia wengine kuwa imara zaidi kwa unachokifanya.
Asante sana kwa kujifunza haya pamoja nami, furaha yangu kuona unatoka hatua moja kwenda nyingine. Nikutakie siku njema yenye mafanikio makubwa.
Ni mimi Rafiki yako Samson Ernest, waweza tembelea Blog hii kujifunza zaidi
www.mtazamowamaisha.blogspt.com
WhatsApp; 0759808081, samsonaron0@gmail.com

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top