MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Sunday, May 3, 2015

Umepata Email? Na Zawadi Nzuri Kwako.

Posted by Makirita Amani  |  at  Sunday, May 03, 2015 No comments

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, naamini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha yako.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wasomaji wote kwa ushirikiano mkubwa na imani kubwa mnayoionesha kwangu na kwa AMKA CONSULTANTS. Jumatatu ya kesho tunakwenda kuanza semina ya mafanikio kwenye biashara, semina ambayo mwisho wa kujiunga ilikuwa jana. Nachukua nafasi hii kuwashukuru sana wasomaji wetu kwa sababu idadi ya waliojiunga na semina ni kubwa kuliko tulivyotegemea awali. Hii inaonesha ni jinsi gani watu wananufaika na kazi kubwa tunayokazana kuifanya kila siku kupitia mitandao yetu mbalimbali.

Kwa idadi hii kubwa ya watu waliojiunga imenifanya nikae chini na kuboresha zaidi mafunzo niliyopanga kutoa. Sio kwamba ya mwanzo hayakuwa mazuri, ila idadi kubwa ya watu waliojiunga imenihamasisha sana na hivyo imenisukuma nitoe mafunzo bora zaidi ya nilivyowahi kufikiri. Naamini kila aliyejiunga ataondoka na kitu kikubwa sana kitakachomwezesha kufanya biashara yake kw autofauti na kufikia mafanikio.

Shukrani hizi nazipelekea kwa wasomaji wote, waliojiunga na hata ambao hawajajiunga. Kwani wale ambao hawajajiunga wamekuwa mabalozi wazuri wamtandao huu kwa kuwashiriksiha wengine na hivyo kuwafikia wengi zaidi.

Nasema asante sana kwa imani hii kubwa na tutaendelea kuwapatia maarifa muhimu yatakayomwezesha kila msomaji kuweza kubadili maisha yake na kuwa bora zaidi.

Kwa wale ambao walijiunga na semina hii tayari imetumwa email ya kwanza ya kudhibitisha ushiriki, tafadhali angalia kama umepata email hiyo. Kama umeipata huna haja ya kujibu, ukishaifungua mfumo wetu utaonesha umefungua. Kama umelipia ili kujiunga na hujapata email tafadhali tuwasiliane mara moja ili uweze kuwekkwa kwenye mafunzo haya. Piga simu au andika ujumbe kwenda namba 0717396253 au 0755953887 mapema ili uweze kupata mafunzo haya mazuri.

Kama hukupata nafasi ya kujiunga mpaka jana, nitaomba sana utusamehe kwani hatutaweza kumuunganisha mtu mwingine. Katika mafunzo mengi yaliyopita tumekuwa tunapokea watu wengi ambao wamechelewa kujiunga na kujiunga baada ya muda kupita. Kwa mafunzo haya ya sasa hatutaweza kufanya hivyo kutokana na mfumo tunaotumia kutoa mafunzo kutoruhusu hali hiyo. Hivyo kama ulikosa nafasi hii ya kujiunga na semina hii unaweza kuendelea kujifunz akupitia mitandao yetu mingine. Na kama hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA fanya hivyo mara moja ili uendelee kujifunza.

Mwisho kabisa naomba nitoe zawadi kwa wasomaji wote kutokana na imani hii kubwa mnayoionesha kwetu. Zawadi hii ni kitabu kizuri sana kinachofundisha kila kitu unachotakiwa kukijua kwenye biashara. Kitabu hiki kinaitwa PERSONAL MBA. Unapomaliza kukisoma kitabu hiki unakuwa sawa na mtu aliyesoma masters ya business administration, yaani shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara. Tena wewe unakuwa na faida kwa sababu umejifunza vitu ambavyo unaweza kuvitumia kwenye biashara moja kwa moja tofauti na yule anayesoma ili kujibu mtihani.

Kitabu hiki kina mambo yote muhimu kuhusu biashara kuanzia kutengeneza thamani kwenye biashara, kutafuta masoko, kutangaza, kutoa huduma nzuri wka wateja na hata usimamizi mzuri wa fedha. Utapata mambo mengi mazuri sana kwenye kitabu hiki. Hiki ni moja ya vitabu ambavyo huwa navisoma mara kwa mara na kila ninaposoma natoka na kitu kipya.

Nisimalize utamu wote wa kitabu hiki, unawez akukipakua wka kubonyeza maandishi haya ya kitabu; PERSONAL MBA.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

 

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top