MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Thursday, April 30, 2015

Hiki Ndicho Kitu Unachotakiwa Kuwa Makini Nacho Sana Ili Kufanikiwa.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Thursday, April 30, 2015 No comments

Inawezekana kabisa katika maisha yako unaweza ukawa unajua ndoto zako vizuri, umeshabaini malengo yako maishani, yaani mambo yaliyokuleta duniani, lakini kuna wakati ukajikuta unakwama kutekeleza mipango na malengo yako uliyojiwekea kutokana na mitazamo yako uliyojiwekea kwenye maisha.
 

Mara nyingi mtazamo ulionao katika maisha yako ndio unaokuamulia upande au ushuke kwa kiasi gani katika maisha. Ili  uweze kupanda juu katika ngazi ya mafanikio na kubaki huko ni lazima uwe na mitazamo thabiti pia itakayokuwa inakuwezesha kuyaangalia maisha kwa namna itakayokupa mafanikio zaidi.

Kuna watu ambao huwa wanamitazamo hasi sana katika maisha yao kiasi kwamba, badala ya kuishi kuzisaka ndoto na malengo waliyojiwekea maishani , wamekuwa ni watu wa kuishi kwa kufuata hofu na woga kila siku. Kuna kauli nyingi ambazo huwa wanajiambia za kujibeza, kuvunja nguvu na kujiona hawafai kwa chochote.

Kwa kuwa na mitazamo hasi, inayopotosha ni kitu ambacho kinaharibu maisha yako kwa sehemu kubwa sana. Ili kuwa na mafanikio makubwa kujiwekea malengo peke yake haitoshi, ni lazima uwe na mitazamo imara itakayokuwa inakuwezesha kusonga mbele hata katika kipindi ambacho kuna hali ya kukata tamaa.


Unapokuwa na mitazamo chanya juu ya kile unachokifanya hakuna kitu kitakachokushinda. Kama ikatokea umekutana na tatizo, kwako halitakiwa tatizo kama wengi watakalivyoliona, bali itakuwa ni changamoto ya kawaida ambayo kwako ni lazima uivuke. Kuwa na mtazamo chanya, hiki ndicho kitu unachotakiwa kuwa makini nacho sana ili kufanikiwa. 

Hakuna mtu au kitu kitachokuzuia kufanikiwa kama utakuwa ndani mwako umejijengea mitazamo chanya na imara. Hata ikitokea watu wakakubeza, kukuzonga, kukutisha na kukuvunja nguvu hiyo itakuwa ni sawa na kazi bure tu kwao, kama wewe tayari unajielewa na una mitazamo sahihi katika maisha yako, hivyo ni lazima ufanikiwe hata iweje.

Kuna wakati huwa tunakutana na changamoto au vikwazo ambavyo huwa vinatufanya tuhisi tena basi, lakini kwa kuwa na mtazamo chanya katika maisha yako haupaswi tena kujiambia na kuamini kuwa utashindwa. Unachotakiwa kufanya ni kukabiliana na hali uliyonayo mpaka kushinda. Hiyo utaweza, kwa kuwa na mtazamo chanya tu, vinginevyo utashindwa.


Kuna wakati unaweza ukajikuta unahofu au unaingia kwenye shughuli ambayo katika hali ya kawaida inakuwa ni ngumu sana kuweza kuitekeleza. Kutokana na ugumu wake au jinsi ilivyo tu inaweza hata ikakukatisha tamaa. Hivyo kwa hali kama hiyo, hakuna kitu kitakachoweza kukufanya ukabiliane nayo kwa ujasiri zaidi ya wewe kuwa na mtazamo chanya wenye matumaini ya kushinda.

Kama nilivyosema awali, unatakiwa kuwa makini sana na mitazamo uliyonayo ili kufika kule unakotaka kufika katika maisha yako. Unapoanguka na kuamua kwamba sasa unataka kusonga mbele na ni lazima usimame, kitu kitakachoweza kukufanya  wewe kuwa imara na kuwa na ujasiri wa kusonga mbele ni mitizamo uliyonayo juu jambo hilo uliloshindwa mwanzo.

Watu wengi wanaoshindwa katika maisha yao mara nyingi ni watu wenye mitizamo hasi sana maishani. Ni watu wenye kuamini sana kutokumudu mambo, pia ni watu wenye kukata tamaa walio na kila aina fikra hasi zinazowakwamisha na kuwarudisha nyuma bila wao hata kujua. Ili watu hawa waweze kubadili hali zao ni lazima kuwa na mitazamo chanya kwao.


Kwa vyovyote vile iwavyo ni muhimu sana kwako kuwa na mtazamo chanya katika maisha yako ili uweze kufanikiwa kwa kile unachokifanya iwe katika biashara ama masomo. Kama hutoweza kumudu kuwa na mtazamo chanya hiyo mara kwa mara itakusumbua na itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufikia mafanikio uliyojiwekea kwako.

Kwa kuweza kubadilisha mtazamo wako kabisa ulionao juu ya biashara na maisha kwa ujumla, unakaribishwa kwenye semina kubwa ya MAFANIKIO katika biashara itakayoendeshwa na AMKA CONSULTANTS kwa njia ya mtandao. Kupata maelezo kamili juu ya semina hiyo ambayo itakuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yako bonyeza hapa.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Tags:
KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top