MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Friday, February 20, 2015

KITABU; The Four Agreements. Kitabu Muhimu Sana.

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, February 20, 2015 No comments

Karibu kwenye utaratibu wetu kushirikishana kitabu ambapo kila mwezi tunashirikishana kitabu kimoja kizuri ambacho kwa kukisoma na kufanyia kazi yale utakayojifunza maisha yako yatabadilika sana.

Kusoma vitabu kuna faida kubwa sana, ukiacha tu kuongeza maarifa, kuna faida nyingi sana unazoweza kuzipata kwa kujisomea vitabu. Katika makala niliyoandika kwenye Makirita Amani hivi karibuni, nimeeleza faida kumi ninazopata kwa kujisomea vitabu ukiondoa kupata maarifa. Baadhi ya faida hizo ni burudani,kupunguza gharama, kuepuka umbea, kuandika na hata kuwa bora zaidi. Faida za kujisomea vitabu haziwezi kufika mwisho.

Kusoma makala hiyo ili na wewe upate kujua manufaa ya kujisomea vitabu fungua hapa;

 Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

Katika utaratibu wetu huu mzuri wa kutumiana vitabu, mwezi huu wa pili mpendwa msomaji utatumiwa kitabu THE FOUR AGREEMENTS kilichoandikwa na Miguel Ruiz.

FOUR AGREEMENTS

Huwa nasema kila kitabu ni kizuri, ila kwa kweli kitabu hiki ni kizuri mno. Nasema ni kizuri mno na ningetamani kila mtu aweze kukisoma. Hii ni kwa sababu kitabu hiki kimejadili yale mambo ya msingi kabisa yanayotengeneza maisha yetu.

Kwanza kabisa mwandishi ameeleza vizuri sana ni jinsi gani sisi tumetengenezwa hivi tulivyo. Yaani hapo ulivyo, kwa hiko unachofanya na hata imani unayoamini hukupenda wewe bali umetengenezwa kuwa hivyo.

Umetengenezwa kuwa hivyo na wazazi, elimu, imani na hata jamii kwa ujumla. Mwandishi ameeleza jinsi ambavyo mfumo wa adhabu na zawadi ulivyotufanya tuwe tulivyo leo.

Katika mfumo huu mzazi anampa mtoto zawadi pale anapofanya kitu anachopenda yeye na anampa adhabu pale anapokwenda kinyume na kile anachoamini mzazi.

Kwa kifupi kuna vitu vingi sana unaweza kujifunza kupitia kitabu hiki. Naweza kusema kitabu hiki kinapaswa kuwa moja ya vitabu muhimu vitakavyobadili mtazamo wako kuhusu wewe mwenyewe na maisha kwa ujumla.

Kama lilivyo jina la kitabu, mwandishi ametushirikisha maazimio manne ya kuishi nayo. Kwa kuishi na maazimio haya tutakuwa na maisha yenye furaha, upendo na mafanikio.

SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

Maazimio manne anayotupa mwandishi ni kama ifuatavyo;

1. Simamia maneno yako.

Hapa mwandishi anatuonesha umuhimu wa kusimamia na kuheshimu maneno yako mwenyewe. Sema kile ambacho unamaanisha na timiza kile unachoahidi. Usikubali kutumia maneno ya kujikatisha tamaa wewe mwenyewe au kushiriki umbea na majungu. Tumia nguvu ya maneno yako katika uelekeo wa ukweli na upendo.

2. Usichukulie jambo lolote kwa ubinafsi.

Hakuna mtu yeyote anayefanya jambo kwa ajili yako binafsi. Kile ambacho wengine wanafanya au kusema ni mtazamo wao wenyewe na sio kwmaba ndio ukweli unaotakiwa kufuatwa na kila mtu. Utakapoweza kujikinga na maoni ya watu wengine utaacha kuwa mwathirika wa mawazo na matendo ya wengine.

Naomba niishie hapa, maana nikieleza maazimio yote manne utakosa hamasa ya kukisoma na kukosa mengi zaidi. Kisome kitabu hiki, utayapata yote hayo kwa undani zaidi na hayo mawili ambayo sijaeleza ni mazuri sana na yatabadili maisha yako kabisa.

Kupata kitabu hiki cha THE FOUR AGREEMENTS bonyeza hayo maandishi ya kitabu na utakipakua.

Pakua kitabu hiki, kisome na anza kuyafanyia kazi yale ambayo unajifunza na nakuhakikishia maisha yako hayataendelea kuwa kama yalivyo sasa. Utapata vitu vichache ambavyo vitafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

SOMA; Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

KARIBU KWENYE KUNDI LA KUJISOMEA;

Kama unataka kujijengea tabia ya kujisomea na ungependa kupata kitu cha kukusukuma uweze kusoma nakukaribisha kwenye kundi la kusoma vitabu. Kundi hili linaitwa VORACIOUS READERS, katika kundi hili tunasoma vitabu viwili kwa wiki na ni muhimu kila mwanachama kusoma na kujadili angalau kitabu kimoja. Kupata maelezo zaidi ya kundi hili bonyeza maandishi haya.

MUHIMU; Usitake kujiunga na kundi hili kwa sababu tu umehamasika, ni muhimu sana utenge muda wa kujisomea na usome kweli, usipofanya hivyo unaondoka kwenye kundi.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.

 

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top