MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Friday, January 16, 2015

Wazo Zuri La Biashara Linachangia Asilimia 1 Tu Ya Mafanikio, Asilimia 99 Inatoka Hapa…

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, January 16, 2015 No comments

Kama ningeweza kupata wazo zuri sana la biashara nina uhakika ningefanikiwa sana. Unajidanganya. Na hivi ndivyo watu wengi sana wanafikiri. Inawezekana unafikiria biashara yako haikupi faida kwa sababu wazo lako la biashara sio zuri. Kila ukiwaangalia wale waliofanikiwa zaidi yako unashawishika kwamba wao wana mawazo mazuri ya biashara kuliko wewe.

Naweza kukumabia kwmaba unatumia sababu ya wazo la biashara kama kisingizio tu cha sababu halisi inayokufanya ushindwe kufanikiwa kwenye biashara.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

 

Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu, tukibadilishana mawazo kuhusu biashara. Katika kuongea akaniambia kwamba ana wazo zuri sana la biashara ila akanisihi nisimwambie mtu wazo hilo maana hataki liibiwe. Baadae alinieleza wazo lake, lilikuwa wazo zuri sana ambalo kwa nafasi aliyonayo angeweza kulifanya vizuri na kufanikiwa sana. Baadae nilimwambia kwamba wala asiwe na woga kuhusu kuibiwa wazo hilo, angeweza hata kumtangazia kila mtu, ila kwa uhakika ni wachache sana ambao wangeweza kulifanya na hata hao ambao wangeweza, hawatakuwa na muda huo maana wako “bize” na kutekeleza mawazo yao mengine.

Ukweli ni kwamba wazo la biashara linachangia asilimia 1 tu ya mafanikio. Yaani hata kama wazo lako lingekuwa bora kiasi gani bado sio uhakika wa kupata mafanikio.

Nina uhakika na hili ninalosema hapa kwa sababu kwa uzoefu tu nimekuwa nawapa watu wengi sana mawazo mazuri ya biashara ila ni wachache sana ambao wanafuata mawazo yale au hata kuyatumia kutengeneza wazo bora zaidi.

Na kama wazo zuri la biashara lingekuwa na uwezo mkubwa zaidi ya hapo katika kuleta mafanikio, wengi sana tungewaona wana mafanikio makubwa.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Asilimia 99 inatoka wapi?

Kama wazo la biashara linachangia asilimia 1 ya mafanikio, je hii asilimia 99 inatoka wapi?

Asilimia 99 ya mafanikio inatoka kwenye kitu kimoja ambacho huenda hutofurahi sana kukisikia. Ni kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakijitahidi kukikwepa ila hakuna njia yoyote ya kuweza kufanya hivyo. Ni kitu ambacho hakiwezi kukwepwa ili kufikia mafanikio, ni kitu ambacho huwezi kutumia nyia ya mkato kufikia mafanikio.

Asilimia 99 ya mafanikio yako itatokana na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kujitoa, kujituma na kutokata tamaa. Hakuna chochote iunachoweza kuwepa kitu hiki muhimu ili kufikia mafanikio.

Unaweza kuwa na wazo zuri sana, ila wazo hilo halitajitekeleza lenyewe. Wazo hilo litakuhitaji wewe ufanye kazi kwa bidii sana. Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi zaidi ya watu wa kawaida wanafanya. Naposema kazi hapa sio lazima iwe kazi ya kutumia nguvu itakayokutoa jasho, ila kazi yoyote ambayo inakufanya uweke juhudi ndio muhimu kufikia mafanikio.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Pamoja na kufanya kazi kwa bidii na maarifa pia utahitaji kujitoa na kujituma sana na kutokata tamaa. Katika wazo lolote zuri la biashara utakalokuwa nalo ni lazima utakitana na changamoto katikati ya safari. Unaweza kuwa na wazo zuri na ukaweka mipango mizuri sana, lakini kumbuka mipango sio matumizi. Unaweza kuweka mipango mizuri lakini kuna vitu vingi sana ambavyo huwezi kuviathiri, kubadilika kwa vitu hivyo kutafanya mipango yako yote ivurugike.

Anza sas akujiandaa zaidi ya kutafuta wazo tu, mafanikio sio wazo zuri, mafanikio ni jinsi gani unaweza kulifanyia wazo hilo zuri kazi. Uzuri ni kwamba kwa dunia ya sasa kuna fursa nyingi sana za kuendeleza wazo lolote na kuweza kutengeneza biashara kubwa itakayokuletea mafanikiomakubwa.

Nakutakia kila la kheri katika mafanikio ya biashara yako.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top