MUHIMU KUSOMA;

SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu, Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikua...

Wednesday, October 29, 2014

Ushauri Muhimu Kwa VIJANA; Okoa Miaka Hii Kumi Ambayo Utaipoteza.

Posted by Makirita Amani  |  at  Wednesday, October 29, 2014 No comments

Katika tafiti mbalimbali zilizofanywa kwenye nchi zilizoendelea miaka ya nyuma, zilikuwa zinaonesha kwamba watu waliofanikiwa sana ni watu wazima. Ilikuwa nadra sana kukuta kijana akiwa na mafanikio makubwa kimaisha na hata kifedha. Ila kwa siku za hivi karibuni mambo yamebadilika kidogo na sasa kuna vijana wengi sana duniani ambao wana mafanikio makubwa kifedha na hata kimaisha. Pamoja na mabadiliko haya bado hapa kwetu Tanzania mambo hayajabadilika sana ndio maana leo nataka tuamshane kama vijana na tuache kupoteza muda.

Ni umri gani wa kufikia mafanikio?

Kama nilivyosema hapo juu, zamani kidogo ilikuwa nadra sana kukuta kijana wa miaka ishirini na akiwa na mafanikio makubwa, hata wa miaka thelathini na walikuwa wa kuhesabika. Watu wengi waliokuwa wamefikia mafanikio makubwa walikuwa kwenye miaka ya arobaini na mwishoni au miaka hamsini na.

Ni nini kilisababisha hali hii?

Kama watu wengi wanaanza kufanya kazi au biashara katika miaka ya ishirini na, kwa nini hawafikii mafanikio mpaka wanapokuwa kwenye miaka ya arobaini mpaka hamsini? Hii ni kwa sababu kuna kipindi ambacho watu wanakipoteza katikati hapo na ndio maana wanachelewa kupata mafanikio.

Katika kipindi cha ujana, vijana wengi hupoteza sio chini ya miaka kumi wakiwa hawajui ni nini wanachofanya, au wakiwa hawapendi kile wanachofanya au wakiwa wanafikiri kuna njia rahisi ya kupata mafanikio.

Kutokujua wanachofanya.

Katika hali hii kijana anakwenda shule kwa sababu wengine wanaenda shule, anasomea ujuzi kwa sababu marafiki zake au jamii imemwambia ujuzi huo ni mzuri. Na baadae anafanya kazi kwa sababu inabidi afanye kazi ndio apate hela ya matumizi. Katika kipindi hiki kijana anapoteza muda mwingi na mafanikio yanakuwa hakuna. Mpaka kijana atakapokuja kujitambua kwamba hajui anachofanya kwenye maisha yake ni nini miaka kumi inakuwa imepita.

Soma; Katika Kula ujana usifanye mambo haya matano, utajutia maisha yako yote.

Kutokupenda wanachofanya.

Changamoto nyingine inayowakabili vijana na kuwafanya wapopteze muda ni kufanya kazi au biashara wasiyoipenda. Kigezo pekee cha kufanya kazi hiyo ni kwa kuwa wameipata au kwa kuwa wanahitaji fedha ya matumizi. Kwa hali hii kijana anakuwa anafanya kazi kama analazimishwa na hivyo hawezi kuonesha uwezo wake mkubwa na hatimaye kupata mafanikio makubwa.

Soma; kama unataka kufanikiwa usifanye kazi 

Kufikiri kuna njia rahisi ya kupata mafanikio.

Changamoto kubwa zaidi inayowakabili vijana ni kufikiri kwamba kuna njia rahisi ya kupata mafanikio kwenye maisha. Kutokana na fikra hizi vijana hujaribu mambo mengi sana na kuacha, muda huu ambao anajaribu mambo mengi anazidi kuupoteza badala ya kuchagua jambo moja na kukomaa nalo. Hili limekuwa linatokea sana, na ndio maana utaona wacheza kamari wengi ni vijana. Akitokea mtu leo akasema kilimo cha mpunga kinalipa, kijana anakimbilia kufanya, kesho akiambiwa kilimo cha nyanya kinalipa sana, anakimbilia tena, baadae anaambiwa kuna biashara nzuri sana na inalipa, anaenda huko pia. Kwa mahangaiko haya kijana anajikuta anapoteza muda mabao kama angechagua kufanya jambo moja au mambo machache angekuwa amepiga hatua sana.

Muda ambao vijana wengi wanapoteza katika hali hizo sio chini ya miaka kumi na kwa kuwa vijana wengi huanza kazi au shughuli nyingine za kiuchumu wakiwa na miaka 25, hivyo mpaka wanafika miaka 35 bado wanakuwa hawajawa na msimamo na maisha yao. Kuanzia hapo au baada ya hapo ndio wanakuwa wameshachoshwa na kazi wasizozipenda au wameshajaribu vitu vingi sana na kuona mambo ni yale yale na hatimaye kuamua kukaa chini na kufanya kitu kimoja au vitu vichache.

Ni muda kiasi gani unahitajika ili kufikia mafanikio?

Tafiti nyingi zinaonesha mtu anahitaji masaa sio chini ya elfu kumi kufanya kile anachokifanya ndio aweze kubobea na kufikia mafanikio makubwa. Kwa ufanyaji kazi wetu wa kazi, masaa elfu kumi ya kufanya kazi kwa umakini suio chini ya miaka kumi, ndio maana watu wengi huja kufikia mafanikio makubwa kwenye miaka ya arobaini au hamsini.

Kijana ufanye nini?

Lengo la kukushirikisha hili ni wewe uokoe miaka hii kumi ambayo unakwenda kuipoteza au umeanza kuipoteza. Chagua ni kitu gani unaweza kukifanya na unapenda sana kukifanya kisha kifanye kwa moyo wako wote na kwa uwezo wako wote, komaa nacho na baada ya muda utaona mafanikio makubwa sana. Acha kusumbuka na kazi ambayo huipendi au haikupeleki popote, acha kujaribu kila kitu unachoambiwa kinalipa, wekeza nguvu zako kwenye kujenga misingi yako ili baadae uwe na maisha yenye mafanikio makubwa.

Dunia ya sasa imebadilika sana, kuwa na mafaniko sio mpaka uwe na kiwanda au uchime mafuta kama ilivyokuwa zamani, hivi sasa kuna fursa nyingi nyingi mno za kukufikisha kwenye mafaniko, ila kwanza ondoa dhana ya kupanda mti leo kesho ule maembe, kila kitu kinahitaji muda.

Pia unahitaji kujifunza kila siku ili kuhamasika na kupata ujuzi zaidi. Nakukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili uanze kujenga safari yako ya mafanikio. Kujua JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi.

Kijana chukua hatua sasa, kabla haujafika wakati ambao utasema NINGEJUA…., ndio umeshajua sasa uamuzi na wako kwamba utafanya nini.

Nawatakia vijana wenzangu wote kila la kheri katika kuyafikia mafanikio.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo432

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top