MUHIMU KUSOMA;

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwekeza Ili Kuweza Kutengeneza Kipato Kwenye Intaneti.

Habari rafiki? Sheria ya asili inasema kila mtu anavuna kile alichopanda, na hiyo ipo wazi kwenye kila jambo tunalofan...

Wednesday, October 8, 2014

TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Kujiamini.

Posted by Makirita Amani  |  at  Wednesday, October 08, 2014 No comments

Karibu tena msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA kwenye kipengele hiki cha KUJIJENGEA TABIA ZA MAFANIKIO. Kwa miezi mitano iliyopita tumejifunza jinsi ya kujijengea tabia muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Tabia tulizojifunza mpaka sasa ni; tabia ya kujisomea, tabia ya kutumia vizuri muda, tabia ya kutunza na kutumia vizuri fedha na tabia ya kujijengea nidhamu binafsi. Hizi zote ni tabia muhimu sana ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Kama huwezi kutumia muda wako vizuri sahau kuhusu mafanikio, muda ndio fedha mpya. Kama hupendi kujisomea nakujifunza zaidi unaweza tu kusahau kuhusu kufikia mafanikio makubwa.

Kama huna tabia nzuri kwenye kutunza na matumizi mazuri ya fedha zako hujui unakoelekea hasa inapokuja kwenye mafanikio. Na kama huna nidhamu binafsi, tafadhali sana usitafute mafanikio makubwa maana utakuwa hatari kwako mwenyewe na kwa wanaokuzunguka.

Sasa tunaingia kwneye kujifunza tabia nyingine muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Tabia hii ni kujiamini na kujithamini. Hii ni tabia muhimu sana itakayokuwezesha kupata mafanikio makubwa na pia kukuwezesha kudumu kwenye mafanikio hayo. Na ukosefu wa tabia hii ndio unafanya watu wengi wanashindwa kuyafikia mafanikio. Kutokujiamini ndio kunafanya watu wengi wanashindwa kwenye biashara. Kutokujiamini ndio kunafanya watu wengi kushindwa kuondoka kwenye ajira zinazowatesa na kwenda kujiajiri.

Ni kutokujiamini ambako kunafanya mtu ashindwe kutumia uwezo mkubwa ulioko ndani yake ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kutokana na umuhimu wa tabia hii na jinsi ukosefu wake umekuwa na madhara makubwa kwenye maisha ya watu wengi, tutajifunza tabia hii kwa miezi miwili. Hivyo kwa mwezi huu wa kumi na mwezi wa kumi na moja kila siku ya jumanne utapata makala moja ya kujifunza kuhusu tabia hii. Utajifunza umuhimu wa tabia hii, jinsi ya kuitengeneza na jinsi ya kuishi nayo. Na pia tutaona uhusiano kati ya tabia ya kujiamini na mafanikio makubwa.

Ili kupata nafasi hii ya kujifunza tabia hizi za mafanikio jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Gharama ya kujiunga ni tsh elfu kumi tu kwa mwaka na utapata nafasi ya kujifunza tabia hizi za mafanikio, kuanzia zilizopita na hata zinazokuja. Pia utapata makala za biashara na ujasiriamali.

Acha kuendelea kusumbuka bila ya kupata mafanikio, karibu upate maarifa haya ambapo utaboresha maisha yako.

Kujiunga nenda kwenye KISIMA CHA MAARIFA jaza fomu na kisha tuma tsh elfu kumi kwa mpesa(0755953887) au tigo pesa/eartel money(0717396253). Chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii ya kujiboresha zaidi.

Twende pamoja katika safari hii ya kujijengea tabia ya kujiamini ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

Mwisho wa makala hizi utapatiwa kanuni ya kujiamini ambayo utaprint na kusaini kisha utakuwa unaisema kila siku asubuhi. Hii itakuwezesha kujenga tabia hii zaidi na pia kufikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio.

TUKO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4323

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top