MUHIMU KUSOMA;

SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu, Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikua...

Thursday, October 16, 2014

Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

Posted by Makirita Amani  |  at  Thursday, October 16, 2014 No comments

Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Na kila mmoja wetu ana lengo la kuwa tajiri au ukipenda kuwa na uhuru wa kifedha. Na lengo hili ndio linatufanya tufanye kazi kwa bidii na maarifa.

Japokuwa watu wengi wanafanya kazi kwa nguvu sana bado maisha yao ni magumu sana. Hii ni kwa sababu hawajui mbinu za kuwafikisha kwenye utajiri.

Leo JIONGEZE na mambo haya matatu na kama ukiyatumia na ukashindwa kuwa tajiri ndani ya miaka 10 ijayo basi wewe hutakuja kuwa tajiri kwenye maisha yako yote. Namaanisha kama utayatumia na kuzingatia ni lazima utakuwa tajiri.

Mambo hayo ni;

1. JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA.

Hii tayari unajua na ndicho unachofanya kila siku. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara ni muhimu kwako kuwa na chanzo cha kukuingizia fedha.

2. JIFUNZE JINSI YA KUTUNZA FEDHA.

Usitumie fedha yote unayoipata. Sehemu ya kipato chako ni mali yako na unatakiwa kuitunza. Jilipe wewe kwanza kwa kuweka pembeni sehemu ya kumi ya kipato chako(asilimia kumi). Sehemu hii ya fedha usiitumie kwenye matumizi mengine yoyote.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kutajirika kwa kuanza na shilingi elfu moja.

3. JIFUNZE JINSI YA KUIFANYA FEDHA IKUFANYIE KAZI.

Sehemu hii ya fedha uliyojiwekea akiba ifanye ikufanye kazi. Iwekeze fedha hii kwenye sehemu ambapo inaweza kukupatia riba na faida unayoipata iwekeze tena.

Ukiweza kufanya mambo hayo matatu kwa nidhamu kubwa NI LAZIMA UTAKUWA TAJIRI na utaacha kuwa na wasiwasi kuhusu fedha.

Kama unaona haiwezekani au hutaki tu kubadili maisha yako endelea hivyo unavyoishi, chaguo ni lako.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia uhuru wa kifedha.

TUPO PAMOJA.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top