MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Tuesday, September 16, 2014

FEDHA: Hii Ndiyo Siri Kubwa Ya Kupata Utajiri Usiyoijua.

Posted by Imani Ngwangwalu  |  at  Tuesday, September 16, 2014 No comments

Kuwa na mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri ni kitu ambacho wengi wanapenda sana kitokee katika maisha yao ingawa wengi huwa sio wawazi. Kama ambavyo umekuwa ukijifunza kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, zipo siri nyingi za jinsi gani unavyoweza kutengeneza pesa zako mwenyewe na hatimaye kuwa tajiri ambazo unaweza ukazitumia kila siku katika maisha yako.


Pamoja na siri hizo muhimu ambazo umekuwa ukijifunza mara kwa mara na zenye uwezo wa kukufanya kuwa tajiri au bilionea kabisa wa kesho, leo katika makala hii nataka nikupe siri moja muhimu na kubwa ambayo pengine unaijua au huijui lakini ukiitumia vizuri itakuletea mafanikio makubwa sana katika maisha yako ya kuelekea kwenye utajiri.

Hii ni siri ambayo nimekuwa nikiitumia katika maisha yangu binafsi na wengine wengi waliofanikiwa huitumia pia na imewasidia sana kufikia malengo makubwa waliyojiwekea. Kama siri hii ya kupata utajiri imefanya kazi kwao na kwako pia itafanya kazi.  Ukiweza kuitumia siri hii vizuri katika maisha yako itakujengea uwezo mkubwa wa kumudu kufanikiwa kwa chochote unachofanya katika maisha yako.

Watu wengi wenye mafanikio wanaijua vizuri siri hii na ndiyo inayowafanya wawe  juu siku zote. Wengi wanaoshindwa kufanikiwa na kujikuta mbio zao nyingi zinaishia kati katika maisha yao ni kutokana na kushindwa kuitumia siri hii vizuri, nami sitaki uwe miongoni mwao nataka uwe mshindi ili tuwe pamoja katika kilele cha mafanikio.

 

Pengine unajiuliza ni siri ipi hasa unayoweza kuitumia na kuleta mafanikio makubwa kwako. Siri hii unayotakiwa kuwa nayo ni siri ya kujikubali mwenyewe na kuamini unaweza kufikia malengo makubwa uliyojiwekea.

Wataalamu mbalimbali wa elimu za mafanikio akiwemo Dr. Vicent Norman Pealle wameeleza hili sana ili uweze kuwa na mafanikio yoyote makubwa ya kimaisha hatua ya kwanza unayotakiwa kuchukua ni kujikubali mwenyewe na kuamini kuwa uwezo huo wa kufanikiwa unao.

Haijalishi watu wengine wanasema nini juu yako iwe kwa mabaya au mazuri, udhaifu fulani au ubora kinachotakiwa ni kujikubali mwenyewe na kuamini unaweza kufikia mafanikio yoyote bila ya kuzuiliwa na kitu chochote kumbuka ndani yako una uwezo mkubwa sana kuliko unavyofikiri.

Wengine wanasubiri mpaka wasifiwe katika nyanja fulani ya maisha ndipo wajikubali wenyewe kuwa wanaweza kufanikiwa na wanapokuwa wanaacha kusifiwa basi kujikubali huanza kufifia pole pole na pengine kufa kabisa. Kitu usichokijua unaposhindwa kujikubali mwenyewe na kuamini kuwa unaweza kufanikiwa unakuwa unazuia mafanikio mengi sana ambayo yangeonekana kwako. Hiyo inakuwa ni sawa na kupoteza maisha yako.

Tatizo walilonalo watu wengi kutokana na mazoea yao au malezi waliyokulia huwa sio rahisi kujikubali wenyewe na kuamini kuwa wanaweza kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa kabisa katika maisha yao. Ni wepesi sana kuwakubali wengine kutokana na yale wanayoyafanya kuliko kujikubali wenyewe. 

Watu wa namna hii mara nyingi huwa sio rahisi kusimama peke yao kwenye maisha na kufanikiwa, kwani wao wanaamini wapo watu wanaoweza zaidi yao kufanikiwa na kujikuta ni watu wa kujishusha tu na kujiweka pembeni na kusubiri hao wanaoweza waweze. Ni kweli kutokana na kutokujikubali kwao hao wanaoweza hujikuta wakiweza kweli huku wenyewe wakijikuta wakiwa ni watu wa kushindwa katika mambo mengi katika maisha yao.

Jiulize mwenyewe binafsi unajikubali na  kujiamini kwa kiasi gani kwamba unaweza kufikia ndoto na malengo yako uliyojiwekea bila ya kuzuiwa na kitu chochote kile. Kama hujiamini ujue kabisa kwako itakuwa ngumu kufikia ndoto zako. Chukua hatua ya kujiamini ili uweze kuishi maisha ya mafanikio unayo tamani kila siku kuyafikia. 

Hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio unayopaswa kuitumia katika maisha yako. Nakutakia ushindi mkubwa katika safari yako ya mafanikio. Endelea kuwashirikisha wengine kujifunza mambo mengi mazuri yanayoendelea katika mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na hakikisha usikose kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa ajili ya kujifunza zaidi na kuweka hazina kubwa itakayokusaidia katika maisha yako yote.

DAIMA TUKO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

IMANI NGWANGWALU – 0767048035/ingwangwalu@gmail.com


Tags:
KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top