MUHIMU KUSOMA;

Biashara Tano Unazoweza Kuanza Kufanya Mwaka 2017 Kwa Mtaji Kidogo Au Bila Ya Mtaji Kabisa.

Popote ambapo utaanza kuzungumza kuhusu biashara, wale ambao hawajaanza biashara watakuambia kitu kimoja; napenda kuanza biashara lakini...

Friday, August 1, 2014

Utaratibu Mpya Wa Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA(MUHIMU SANA KUSOMA)

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, August 01, 2014 No comments

Kutokana na idadi kubwa ya watu na pia kutokana na changamoto nyingi zilizotokana na mfumo wa awali wa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA sasa yamefanyika marekebisho ambayo yataboresha sana mfumo wa uendeshaji wa KISIMA CHA MAARIFA.
Mabadiliko haya yataathiri wanachama wote waliojiunga mwanzo na wanaoendelea kujiunga. Hivyo nawaomba sana wale wote ambao walishajiunga na KISIMA CHA MAARIFA kusoma hapa kwa makini ili kuweza kufanya mabadiliko.
Kwa nini kubadili mfumo.
Kuna sababu nyingi zilizopelekea kubadili mfumo. Baadhi ya sababu hizo ni;
1. Idadi ya wanachama kuwa wengi hivyo mfumo wa zamani kushindwa kuhimili.
2. Uwezekano wa walio nje ya nchi kulipia kwa pay pal. Mfumo wa mwanzo haukuwa unaruhusu hili na hivyo watu wengi walioko nje ya nchi walikuwa wakishindwa kujiunga.
3. Kumwezesha kila mtu kupata mafunzo ya ndani ya KISIMA. Kama utakumbuka nilitoa taarifa kwamba kwanzia mwezi huu wa nane gharama za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA zinaongezeka. Baada ya kutoa taarifa ile watu wengi waliniandikia kusema wanapenda kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ila gharama ikiongezeka itakuwa kikwazo kwao. Kwa kuwa napenda kila Mtanzania na mtu mwingine mwenye kupenda kupata mafanikio asome KISIMA CHA MAARIFA nimeweka aina tatu za uanachama ambapo mtu anaweza kuchagua ajiunge na uanachama upi. Mfumo wa mwanzo haukuweza kuruhusu hili.
Mfumo mpya wa KISIMA CHA MAARIFA.
Kupitia mfumo huu mpya wa uanachama kutakuwa na mambo yafuatayo;
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuna uanachama wa aina tatu.
1. BRONZE MEMBER, kupitia uanachama huu utaweza kusoma makala mbili kila wiki, moja ya KUJENGA TABIA ZA MAFANIKIO na nyingine ya BIASHARA/UJASIRIAMALI. Pia utaweza kuingia kwenye FORUM na kusoma au kuchangia mada mbalimbali.
Ada ya kujiunga na uanachama huu ni tsh elfu kumi(10,000/) na ni ada ya mwaka mmoja.
2. SILVER MEMBER, kupitia uanachama huu utaweza kusoma makala za, TABIA ZA MAFANIKIO, UJASIRIAMALI/BIASHARA na UCHAMBUZI WA VITABU. Pia utaweza kuingia kwenye FORUM tatu na kuachangia au kusoma.
Ada ya uanachama huu ni tsh elfu thelathini(30,000/=) na ni ada ya mwaka mmoja.
3. GOLD MEMBER, kupitia uanachama huu utaweza kusoma makala; TABIA ZA MAFANIKIO, UJASIRIAMALI/BIASHARA, UCHAMBUZI WA VITABU,  WORLD CLASS PERFORMANCE na KUDOWNLOAD AUDIO BOOKS NA VIDEOS. Pia utaweza kuingia kwenye forum nne na kuchangia au kusoma.
Ada ya uanachama huu ni tsh elfu hamsini (50,000/=) kwa mwaka mmoja.
JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA jaza fomu ya kujiunga kwa kuweka taarifa zako sahihi.  Baada ya kujaza fomu nenda kwenye email yako na utakuta taarifa zako utakazotumia kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Utaweza kulog in kwenye KISIMA CHA MAARIFA ila hutaweza kusoma makala yoyote mpaka utakapolipia uanachama.
Kulipia uanachama tuma fedha ya uanachama unaotaka kujiunga(BRONZE-10,000/= SILVER-30,000/= au GOLD-50,000/=) kwenda kwenye namba zifuatazo; MPESA 0755953887, TIGO PESA 0717396253 Kama una AIRTEL MONEY unaweza kutuma moja kwa moja kwenye namba ya tigo-0717396253.
Ukishatuma fedha hizo utatuma ujumbe wenye jina lako na email yako kwenye moja ya namba hizo ili uweze kuwekwa kwenye uanachama husika.
BONYEZA HAPA KUJAZA FOMU YA KUJIUNGA
Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambapo utajifunza mambo mengi sana yatakayokuwezesha kufikia MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE MAISHA YAKO.
KWA WANACHAMA ZA ZAMANI.
Wanachama wote ambao walijiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 01/08/2014 watapata ofa ya kuingia moja kwa moja kwenye uanachama wa SILVER. Kwa wewe ambaye tayari ulikuwa mwanachama bonyeza kujaza fomu ya kujiunga hapo juu kisha weka taarifa zako na baada ya kujiunga nitumie ujumbe kwenye namba za simu wenye email yako uliyojiunga nayo zamani kisha utapata nafasi ya uanachama wa SILVER.
OFA MAALUMU YA MUDA MFUPI.
Kwa wiki hii ya kwanza ya mwezi wa nane uanachama wa SILVER unaweza kuupata kwa punguzo la ada, badala ya tsh elfu thelathini utalipa elfu ishirini. Mwisho wa ofa hii ni ijumaa tarehe 08/08/2014. Wahi nafasi hii nzuri ya kupata mambo mazuri yatakayoboresha maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako.
TUKO PAMOJA.
kitabu-kava-tangazo432

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top