Tuko kwenye nusu ya pili ya mwaka huu 2014. Pamoja na kumaliza nusu ya mwaka huu, kuna mambo mengi ulipanga kufanya ila hujaweza kukamilisha. Sababu kubwa iliyokufanya ushindwe kufanya mambo hayo ni jinsi ulivyopangilia kufanya. Kuna makosa mengi sana ambayo watu wengi wamekuwa wanayafanya wakati wa kuweka malengo. Umekuwa ukirudia makosa hayo kila mwaka na ndio maana umeshindwa kufikia malengo makubwa.
Wiki ijayo nakuletea mafunzo kwa njia ya email ambayo yamejikita katika kukuwezesha kuweka malengo amkubwa ambayo utayafikia. Katika mafunzo haya utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka malengo hayo makubwa na yanavyoweza kuwa na maana kwako na ukaweza kuyaishi kila siku.
Mafunzo haya tuliyafanya tena mwezi wa kwanza na yalikuwa na mafanikio makubwa sana kwa washiriki. Sasa unapata nafasi ya pekee ya kupata tena mafunzo haya ili uweze kufanya jambo kubwa kabla mwaka huu 2014 haujaisha.
Mafunzo haya yatatolewa kwa njia ya email kwa siku tano mfululizo. Mafunzo yataanza jumatatu tarehe 7/07/2014 mpaka ijumaa tarehe 11/07/2014. Kila mshiriki atatumiwa email moja kwa siku iliyochambuliwa na kuelezwa vizuri sana somo husika. Mshiriki ataweza kuuliza swali kwa kujibu email au kupiga simu. Pia mshiriki atakuwa akipewa maswali machache ili kujua kama anafuatilia mafunzo vyema.
Mafunzo yatatolewa hivi;
1. Jumatatu; Umuhimu wa kuweka malengo na lengo kuu la maisha ambalo kila mtu analipigania, hata wewe.
2. Jumanne; Aina tano za malengo unayotakiwa kuweka kwenye maisha yako.
3. Jumatano; Hatua saba za kuweka malengo ambapo lazima utayafikia.
4. Alhamisi; Makosa makubwa unayoyafanya na ambayo umekuwa ukiyarudia unapoweka malengo na jinsi ya kuyaepuka.
5. Ijumaa; Unafanya nini baada ya hapa? Unaanzia wapi?
Gharama ya mafunzo ni tsh 5,000/= na italipwa kwa njia ya Mpesa(0755953887), Tigo pesa(0717396253). Mwisho wa kulipia ada ya tsh 5,000/= ya mafunzo haya ni leo ijumaa tarehe 4/07/2014 baada ya hapo utalipia ada ya tsh 10,000/=. Chukua hatua sasa kabla muda haujakwisha.
Unafikiri 2014 haiwezekani tena? Pata mafunzo haya na ufanye jambo ambalo baadae utajishukuru sana.
Nakukaribisha katika mafunzo haya ambayo yatabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa.
TUKO PAMOJA.
