MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Friday, May 16, 2014

KITABU; The Science Of Getting Rich(Sayansi Ya Kuwa Tajiri)

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, May 16, 2014 No comments

Kama ulivyo utaratibu wa mtandao wa AMKA MTANZANIA kila mwezi wewe msomaji unatumiwa kitabu kizuri cha kujisomea. Kitabu hicho kinakuwa na mbinu mbalimbali za kuweza kukusaidia kuvuka changamoto unazokutana nazo au kutumia fursa zinazokuzunguka ili kufikia mafanikio makubwa kimaisha.

Vitabu unavyotumiwa ni vitabu ambavyo watu wengi duniani wamekiri kubadilisha maisha yao kwa kusoma vitabu vya aina hii. Hivyo na wewe msomaji kama unasoma vitabu hivi ni lazima maisha yako yatabadilika na kuwa bora zaidi, ILA TU KAMA UTACHUKUA HATUA YA KUFANYA YALE UNAYOJIFUNZA.

Mwezi huu wa tano nakutumia kitabu THE SCIENCE OF GETTING RICH kilichoandikwa na WALLES D. WATTLES.

sayansi utajiri

Hivi unajua kwamba kuna sayansi ya kupata utajiri? Huenda hujui hilo, na sio kosa lako kwa sababu hakuna sehemu yoyote kwenye mfumo wa elimu au kwenye maisha ya kijamii unafundishwa sayansi hii. Unashangaa kwa nini umesoma, unafanyakazi kwa bidii, umeanzisha na biashara ila bado hufikii utajiri unaotazamia?  Unashangaa kwa nini kuna watu wanaonekana ni wa kawaida sana ila wanapata mafanikio makubwa sana kifedha kuliko wewe? Kuna sayansi ya utajiri ambayo mpaka sasa wewe hujaijua.

Watu wachache sana wanajua sayansi hii ya kupata utajiri ila pia hawapo tayari kuwafunsisha wengine ndio maana jamii imejaa watu wengi ambao wanahangaika kupata utajiri ila hawaupati.

Sayansi hii sio ya kufanya maabara au kutumia nguvu za miujiza, bali ni mambo ambayo unaweza kuanza kufanya leo na maisha yako yakabadilika kwa kiwango kikubwa sana.

Kupitia kitabu hiki utajifunza njia mbalimbali za kutengeneza na kuendeleza utajiri wako. Kupitia kitabu hiki utajifunza mbinu ambazo kama ukizitumia utajiri utakufuata wewe badala ya wewe kuukimbiza na kuishia kuchoka bila kuupata.

Kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwenye kitabu hiki. Nakushauri sana ukisome kitabu hili.

Kwa wale wavivu wa kusoma najua umeshaanza kusema huna muda wa kukisoma. Sasa ngoja kwa kifupi sana nikuoneshe ni jinsi gani unaweza kukisoma kitabu hiki bila ya kutumia nguvu au kubadili ratiba zako.

Kitabu hiki kina kurasa 64, ila kurasa zenye maandishi unayotakiwa kusoma ni 51. Kwa kurasa hizi 51 kama umepanga kuzisoma ndani ya mwezi mmoja(siku30) ina maana kwa siku soma kurasa mbili tu ambazo hazitakuchukua hata dakika tano. Kwa mpango huu utajifunza mambo mengi sana.

Kitabu hiki kimetumwa kwa wanachama wa mtandao wa AMKA MTANZANIA. Kama unataka kupata kitabu hiki na bado hujawa mwanachama wa AMKA MTANZANIA bonyeza maandishi haya na uweke email yako, baada ya kukamilisha kujiunga utatumiwa email yenye link ya kitabu hiki. Bonyeza link hiyo na utaanza kudownload kitabu hiki mara moja.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka hakuna kitu chochote au mtu yeyote anayeweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa unayotazamia, ni wewe mwenyewe tu.

TUKO PAMOJA KWENYE SAFARI HII.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top