MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Monday, April 14, 2014

Kwa Wasomaji Wapya Wa AMKA MTANZANIA; Karibu Sana na Soma Hapa.

Posted by Makirita Amani  |  at  Monday, April 14, 2014 1 comment

Baada ya kipindi cha AMKA NA BADILIKA jana jumapili kupitia TBC1 tumepata ongezeko kubwa sana la wasomaji wapya kwenye mtandao wetu wa AMKA MTANZANIA. Kwa wewe tu kuwa msomaji wa mtandao huu tayari umeshakuwa sehemu ya mtandao huu na ni wako. Utumie mtandao huu uweze kukusaidia kufikia ndoto kubwa kwenye maisha yako. Ili uweze kutumia mtandao huu vizuri kuna vitu vichache vya msingi unatakiwa kuvifahamu.

amka na badilika2

1. AMKA MTANZANIA ni nini?

Amka Mtanzania ni mtandao(blog) inayotoa mafunzo na kuwahamasisha watanzania kuchukua hatua juu ya maisha yao. Kupitia AMKA MTANZANIA tunapeana mawazo chanya na kuhamasishana kutokata tamaa wala kulalamika. Naamini kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa na vipaji vya kipekee. Kwa kuweza kutumia vitu hivi ukichanganya na mazingira unaweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

2. Nawezaje kunufaika na AMKA MTANZANIA.

Kupitia Amka Mtanzania utaweza kupata mafunzo na taarifa mbalimbali za kukufundisha na kukuhamasisha wewe kuchukua hatua na kuboresha maisha yako. Ili kuweza kujifunza vizuri kila siku soma makala chache kwenye Amka Mtanzania kisha anza kutumia kile ulichojifunza kwenye kazi au biashara zako. Kuna makala zaidi ya 250 ndani ya mtandao huu, na zote ni nzuri mno. Ukitaka uzimalize zote kwa muda mchache utapata taarifa nyingi sana halafu utashindwa kujua uanzie wapi. Anza kidogo, jifunze, tekeleza. Unaweza kuanza kwa kusoma makala hizi kumi zilizosomwa sana mwaka 2013(bonyeza hayo maadishi kuzisoma)

3. Kuacha makala hizi nzuri ni kipi cha ziada kutoka AMKA MTANZANIA.

Kama umesoma AMKA MTANZANIA utaona ni blog ya kipekee. Kupitia AMKA MTANZANIA kuna blog nyingine inaitwa KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA utajifunza mengi na kwa undani zaidi kuhusu mafanikio kwenye kazi na biashara na pia maisha kwa ujumla. Pia utapata nafasi ya kujifunza mambo ya teknolojia ya internet ambayo ni muhimu sana kwa mafanikio ya karne hii. Ili kujiunga na kisima unatakiwa kutuma fedha tsh elfu kumi kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 na kisha unatuma email yako halafu unaunganishwa na kisima. Kwa maelezo zaidi kuhusu KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi haya.

  Pia kupitia AMKA MTANZANIA unapata kitabu kinachoitwa KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI, SABABU ISHIRINI NA TANO ZINAZOKUZUIA WEWE KUFIKIA UTAJIRI. Kitabu hiki kinaelezea tabia ambazo tunapenda kuzifanya ambazo zinatufanya tuendelee kuwa masikini. Pata kitabu hiki na uanze kubadili muelekeo wa maisha yako. Ni kitabu ambacho hutakiwi kukikosa kama unamipango mikubwa kwenye maisha yako. Kitabu hiki kinapatikana kwa soft copy(PDF) kwa tsh elfu tano na unatuma fedha kwenda 0717396253/0755953887 na unatuma email yako kisha unatumiwa kitabu. Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki bonyeza maandishi haya.

4. Nawezaje kuwa sehemu ya AMKA MTANZANIA.

Kwa kusoma makala kwenye AMKA MTANZANIA tayari wewe ni sehemu ya AMKA MTANZANIA. Utakamilisha uwepo wako kwenye AMKA MTANZANIA kama utawashirikisha wengine na kuwaalika nao kutembelea AMKA MTANZANIA ili nao waweze kupata mambo haya mazuri. Pia kama una hadithi nzuri ambayo unadhani inaweza kuwasaidia watanzania wenzako unakaribishwa kutushirikisha. Kama unataka kuandika kwenye mtandao huu karibu sana uweze kutushirikisha. Kuweza kuandika au kutupa hadithi yako tafadhali wasiliana nami kupitia 0717396251/amakirita@gmail.com

  Nakushukuru sana wewe msomaji wa AMKA MTANZANIA. Nakusihi sana tuendelee kuwa pamoja mpaka kila mmoja wetu atakapofikia malengo mkubwa aliyojiwekea. Na hata baada ya kufikia malengo tuendelee kuwa pamoja ili tuzidi kuboresha maisha yetu.

  Nakukaribisha sana katika safari hii ya kuboresha maisha yetu. Kumbuka wewe ndio dereva wa maisha yako. Kama utaamua kufika safari yako au ukaamua kuishia barabarani huo ni uamuzi wako. Nakusihi twende pamoja kwenye safari hii.

Nakutakia kila la kheri, KUMBUKA TUKO PAMOJA.

Makirita Amani,

Mwendeshaji mkuu wa AMKA MTANZANIA

0717396253

amakirita@gmail.com

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

1 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top