MUHIMU KUSOMA;

SEMINA; Elimu Ya Msingi Ya Fedha (Basic Financial Education).

Habari za leo rafiki yangu, Mwanzoni mwa mwaka huu 2017 niliendesha semina yetu ya kwanza ya mwaka 2017 kwa njia ya mtandao. Na nilikua...

Friday, April 11, 2014

Kitabu; Richard Branson–Mafunzo Ya Maisha(Screw It, Lets Do It).

Posted by Makirita Amani  |  at  Friday, April 11, 2014 No comments

Mwezi huu tutajisomea kitabu kilichoandikwa na Richard Branson kinachoitwa SREW IT, LETS DO IT, LESSONS IN LIFE.

  Richard Branson ni bilionea wa kiingereza ambaye utajiri wake unakadiriwa kufikia dola bilioni 5. Richard ni mwanzilishi na mwendeshaji mkuu wa kundi la makampuni lijulikanalo kama Virgin Group. Katika kundi hili anamiliki makampuni zaidi ya 400. Ni kitu cha kipekee sana kwa mtu mmoja kuweza kuendesha makampuni 400 yenye wafanyakazi zaidi ya 16,000.

RICHARD BRANSON 3richard branson

  Richard Branson alianza ujasiriamali akiwa na miaka 16 baada ya kuacha shule. Kilichomfanya aache shule ni kutokana na tatizo la kushindwa kuelewa, yani alikuwa mzito sana kuelewa darasani. Anasema mwalimu mkuu wa shule yake alimwambia atakuwa bilionea au ataishia jela.

  Baada ya kuacha shule Richard alianzisha jarida lake ambalo alikuwa akiandika mambo yanayohusu wanafunzi. Baadae alifungua studio ya kurekodi muziki na biashara zake zikaendelea kukua mpaka kufikia makampuni zaidi ya 400.

  Katika kitabu hiki Screw It, Lets Do It, Richard anaelezea misingi aliyosimamia kwenye maisha yake na ikamuwezesha kufikia mafanikio makubwa aliyonayo sasa. Misingi hiyo sio siri kubwa sana bali ni mambo ya kawaida ambayo hata mimi na wewe tunaweza kuyafanya na tukafikia mafanikio makubwa.

  Moja ya misingi aliyosimamia ni; Kufanya tu(Just Do It). Katika kufanya tu, Richard anakushauri yafuatayo;

1. Amini kwamba inawezekana

2. Kuwa na malengo

3. Ishi maisha yako

4. Usikate tamaa

5. Jiandae vizuri

6. Jiamini

7. Wasaidie na wengine.

Misingi mingine anayotufundisha Richard ni;

Kuwa na furaha, Jipe changamoto, Simama kwa miguu yako, Ishi wakati huu, Thamini familia na marafiki, Kuwa na heshima, Fanya mambo mazuri.

  Kitabu hiki ni kifupi sana na unaweza kukisoma na kukimaliza ndani ya masaa mawili. Ni kitabu ambacho kitakupa mafunzo makubwa sana kuhusu maisha na mafanikio.

  Nakusihi sana ukisome kitabu hiki kwani kitakuwa na msaada mkubwa kwako. Hata kama hujawahi kusoma kitabu kingine chochote nilichowahi kutuma, tafadhali sana soma kitabu hiki tu. Kitakufungua na kukuonesha kwamba hakuna lisilowezekana.

  Kitabu hiki kimetumwa kwa wanachama wa mtandao wa AMKA MTANZANIA. Kama hujakipata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na uweke email yako kisha utatumiwa email yenye link ya kitabu papo hapo, ni bure kabisa.

  Nakutakia kila la kheri katika harakati zako za mafanikio.

Kumbuka Tuko Pamoja.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

0 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top