MUHIMU KUSOMA;

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Habari rafiki? Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina ...

Wednesday, April 9, 2014

Kama Una Tabia Hizi 30 Tayari Wewe Ni Mjasiriamali, Chukua Hatua.

Posted by Makirita Amani  |  at  Wednesday, April 09, 2014 3 comments

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkubwa ikiwa mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa. Kwa kuangalia tabia za wajasiriamali na tabia za binadamu kwa ujumla, wajasiriamali wana tabia za kipekee. Wajasiriamali wanafikiri tofauti na wanatenda tofauti na watu wengine kwenye jamii.

Tabia za kipekee zinazooneshwa na wajasiriamali kuna ambao wamezaliwa nazo na kuna ambao wamezipata kutoka kwenye mazingira na shughuli wanazofanya.

Hapa nitaelezea tabia thelathini(30) ambazo ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali. Kama huna tabia hizi unaweza ukaanza kujifunza taratibu na baadae ukawa na tabia za kijasiriamali. Kumbuka tofauti kubwa ya mjasiriamali ni jinsi anavyofikiri na kuchukua hatua tofauti na watu wengine. Kwa mfano wakati mwajiriwa anaweza kukubaliana na shida anazopata kwenye ajira yake na kuona hakuna anachoweza kufanya, mjasiriamali anafikiria uwezo wa tofauti alionao na jinsi anavyoweza kwenda kuutumia nje ya ajira na akafanikiwa. Baada ya hapo anaweza kuacha kazi na kwenda kufanya lile litakalomridhisha. Kwa kuwa na mtizamo chanya na utayari wa kuchukua hatua kunawafanya wajasiriamali kupata mafanikio makubwa.

ujasiria

Kama unatabia hizi 30, ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali, unatakiwa kuchukua hatua mara moja ili kufikia mafanikio makubwa;

1. Hukubaliani na mfumo. Mara nyingi umekuwa ukihoji kwa nini kitu fulani kifanyike na umekuwa ukijitahidi kutafuta njia bora zaidi ya kufanya kazi fulani pale unapokuwa umeajiriwa. Hufanyi kitu bila ya kuhoji umuhimu wake na kufikiri njia ya kuboresha.

2. Unaonekana kama mfanyakazi mkorofi. Wakati mwingine umeshafukuzwa kazi mara kadhaa kutokana na tabia yako ya kuhoji na kutaka kuboresha utendaji kazi. Au umeshaacha kazi au kupanga kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na kazi hiyo.

3. Una hamasa kubwa ya kutekeleza majukumu yako. Husubiri upangiwe cha kufanya, unajua majukumu yako na unayafanya kwa ubora wa hali ya juu.

4. Ukiambiwa hapana huridhiki, hapana sio jibu kwako unaendelea kutafuta njia nyingine mpaka upate NDIYO.

5. Unajiamini na unaamini una uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa. Una uhakika hata kitokee kitu gani bado unauwezo wa kusimama na kuleta tofauti.

6. Ni mtu wa watu, unaweza kuchangamana na watu wa aina zote. Huna ubaguzi wa aina gani ya watu unaweza kukaa nao, popote unapokutana na watu unaweza kuanzisha mazungumzo na mkaenda vizuri.

7. Huogopi sana juu ya usalama wa ajira kwani unaamini hata bila ya ajira bado unaweza kuendesha maisha yako.

8. Mara kadhaa umekuwa ukigomea mamlaka. Umekuwa ukikataa maelekezo yanayotolewa na mamlaka kama hayaendani na misimamo yako ya ufanyaji kazi bora. Hii imekupelekea kuonekana ni mfanyakazi mkorofi na hata kufukuzwa.

9. Siku za mapumziko kama sikukuu au mwisho wa wiki ndio siku bora kwako kufanya kazi zako binafsi, huendekezi kupoteza muda kwa kupumzika au kustarehe.

10. Umewahi kuuza vitu vidogo vidogo ulipokuwa mtoto. Pia umewahi kufuga kuku, sungura na hata njiwa enzi za utoto wako.

Endelea kusoma tabia nyingine 20 za ujasiriamali kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Ndani ya kisima utajifunza mengi kuhusu mafanikio kwenye biashara na maisha kwa ujumla. Kupata maelekezo ya kujiunga na kisima bonyeza hayo maandishi ya jina.

KUHUSU AMKA MTANZANIA

AMKA MTANZANIA ni mtandao unaokuhamasisha wewe mtanzania kuchukua hatua juu ya maisha yako. Kupitia mtandao huu utajifunza na kuhamasika ili uweze kuchukua hatua ya kufikia mafanikio makubwa. Kama unataka kutumiwa makala nzuri na vitabu moja kwa moja kwenye email yako, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu. KARIBU SANA UJIFUNZE NA KUHAMASIKA

Pata Makala Inapotoka

Weka email yako hapa na uwe wa kwanza kupata makala nzuri inapowekwa kwenye mtandao huu.

Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri

Makala Zinazohusiana na Hii

3 comments:

USIACHE KUWEKA MAONI YAKO HAPA.

© 2013 AMKA MTANZANIA. WP Theme-junkie converted by BloggerTheme9
Blogger templates | Distributed By: BloggerBulk Proudly Powered by Blogger.
back to top