Kutokana na mihangaiko ya kila siku kuna badhi ya watu wanajikuta hawana ratiba ama utaratibu wa kupata kifungua kinywa. Wengine wanaacha kupata kifungua kinywa makusudi kwa lengo la kupunguza uzito na kuna wengine wanakosa kifungua kinywa kwa sababu za kifedha.
Inawezekana pia kutokana na shughuli zako nyingi ama ratiba zako unachelewa sana kupata kifungua kinywa.
Bila ya kujali ni sababu gani inayoufanya usipate ama uchelewe kupata kifungua kinywa kuna matatizo ya kiafya yanaweza kukupata kwa kutopata kifungua kinywa.
Utafiti iliofanywa nchini marekani unaonesha kwamba kutopata kifungua kinywa kunaweza kusababisha shinikizo la damu, kuongezeka uzito, na kungezeka kwa mafuta kwenye damu.
Utafiti huo ulihusisha wanaume 27,000 wenye miaka kati ya 45-82 na ulifanyika kwa miaka 16. Utafiti ulihusisha mitindo ya maisha kama kutokupata kifungua kinywa na magonjwa ya moyo.
Majibu yananesha kwamba wanaume wasiopata kifungua kinywa wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 27.
Watafiti hao wanasema chanzo cha magonjwa ya moyo kutokana na kukosa kifungua kinywa ni mfungo wa muda mrefu unaosababisha mwili kushindwa kufanya kazi vizuri. Tunapolala usiku tunakuwa tumefunga(hatuli usingizini) kama unapoamka huli chochote ina maana unaendeleza mfungo kitu ambacho kinauchosha mwili na kushindwa kuunguza mafuta yaliyopo kwenye damu. Kutokuvunjwa kwa mafuta hayo ndio chanzo cha magonjwa ya moyo na kuongezeka uzito/unene.
Tatizo hilo la mwili kuchoka pia linatkea pale mtu anapochelewa kupata kifungua kinywa, hivyo inashauriwa kifungua kinywa kipatikane mapema asubuhi ili mwili uweze kufanya kazi zake vizuri.